Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,Mhe.Joseph Kakunda amewataka viongozi wa Serikali Wilayani Handeni kuhakikisha wanasimamia vyema fedha za miradi ya maendeleo.
Hayo ameyasema wakati za ziara yake baada ya kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa kwenye maeneo hayo,maeneo aliyotembelea ni Ujenzi wa maabara katika Shule Sekondari Kileleni,ujenzi wa jengo jipya la Utawala la Halmashauri ya Mji Handeni,darasa,choo pamoja na mabweni yanayojengwa katika Shule ya Sekondari Handeni.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo Mhe.Kakunda amesisitiza kuwa Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kuhakikisha Wananchi wanaondokana kero mbalimbali kwenye sekta muhimu yaani Afya na Elimu ambazo kwa namna moja au nyingine zinagusa kwa kiasi kikubwa maisha ya Wananchi wengi.
Kwa upande wa Elimu mpaka sasa Serikali imezifikia jumla ya Shule za msingi 6200 na Shule za Sekondari 3159 Nchi nzima kwenye masuala ya ujenzi wa madarasa, mabweni, matundu ya vyoo, nyumba za Walimu, mabweni pamoja na mabwalo. vile vile Serikali imeendelea kuhakikisha inawapatia motisha pamoja na nyenzo zinatakazo saidia utendaji kazi kwa watumishi wa sekta ya Elimu.
"Mpaka sasa nchi nzima Wakuu wa Shule, Walimu Wakuu, na Maafisa Elimu Kata wote Nchini wanapewa posho ya madaraka kila mwezi nje ya mshahara, vile vile Maafisa Elimu Kata Nchi nzima wamepatiwa pikipiki kwa ajili ya kurahisisha ufuatiliaji wa masuala ya Elimu katika maeneo yao hiki sio kitu kidogo bahati nzuri Wananchi wanaona, " amesema Kakunda.
Kwa upande wa Afya Serikali imeendelea kuongeza bajeti ya vifaa tiba na dawa mwaka hadi mwaka, kwa mfano bajet ya vifaa tiba imeongezeka mpaka takibrani bilioni 270 toka bilioni 35 toka mwaka 2015.Vile vile juhudi za ujenzi wa vituo vya Afya imekuwa ikiendelea kwa kasi toka Serikali ya awamu ya tano iingie madarakani jumla takribani miaka 2 inatarajia kujenga jumla ya vituo vya Afya 205.
Mhe.Joseph Kakunda Naibu Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI akiwasili katika Shule ya Sekondari Handeni wakati wa ziara yake tarehe 17/08/2018
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Handeni wakifuatilia hotuba ya Mhe.Joseph Kakunda Naibu Waziri OR-TAMISEMI alipofanya ziara Shuleni hapo tarehe 17/08/2018
Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe.Twaha Mgaya (wa kwanza kushoto) akifafanua jambo mbele Naibu Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI Mhe.Joseph Kakunda
Barabara ya Korogwe - Handeni
Anuani ya Posta: S.L.P 51 HANDENI
Simu ya Mezani: 027-2641807
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: td@handenitc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.