KITENGO CHA SHERIA
MAJUKUMU YA KITENGO.
1. Kutoa ushauri kwa Halmashauri ili kufikia maamuzi mazuri ambayo humaliza migogoro.
2. Kutunga sheria ndogo za Halmashauri
3. Kuandaa miswada ya sheria ndogo za Mitaa kulingana na mahitaji ya Halmashauri au kufuatana na maelekezo tunayopokea.
4. Kuhudhuria kesi mbalimbali Mahakamani zinazoihusu Halmashauri ya Mji na na kutoa utetezi kwa mujibu wa sheria (Legal Advocacy Defence)
5. Kutoa taarifa mbali mbali za migogoro ya kisheria inayoihusu Halmashauri.
6. Kusaidia Kutatua migogoro mbalimbali inayowakabili wananchi baina ya wao wenyewe au Serikali za Mitaa kwa mujibu wa sheria za Nchi.
7. Kuhimiza na kusimamia utawala wa sheria ndani ya Halmashauri na katika serikali za vijiji ili kuhakikisha kuwa haki inatendeka na migogoro kumalizika.
8. Kufuatilia misuada, waraka au marekebisho ya sheria zinazohusu maslahi ya Halmashauri na kutoa taarifa kwenye Halmashauri kwa wakati.
9. Kufanya upekuzi wa mikataba mblimbali ya manunuzi katika Halmashauri.
Barabara ya Korogwe - Handeni
Anuani ya Posta: S.L.P 51 HANDENI
Simu ya Mezani: 027-2641807
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: td@handenitc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.