Hospitali ya Wilaya Handeni imepokea vifaa vya kutolea Huduma kwa watoto njiti kutoka kwa taasisi ya Dorice Mollel Foundation.
Hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika eneo la hospitali ya Wilaya ambapo mgeni rasmi alikuwa ni mhe.Godwin Gondwe Mkuu wa Wilaya ya Handeni, akizungumza wakati wa makabidhiano DC Gondwe ameishukuru taasis hiyo kwa kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Dkt John Pombe Magufuli katika Sekta ya Afya ambapo Serikali imekuwa ikitatua kero katika sekta hiyo kwa kuongeza bajeti ya dawa na vifaa tiba.
Vifaa hivyo vina thamani ya zaidi ya tshs milioni 20, akizungumza wakati wa hafla hiyo Mkurugenzi wa foundation bi Dorice amesema haikuwa rahisi kwa taasisi hiyo kupata vifaa hivyo kwa sababu bei yake ni kubwa sana hivyo basi anaomba vitunzwe vizuri ili viweze kutoa huduma hiyo kwa walengwa.
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji Handeni Dr Feisal Said amesema ujio wa vifaa hivyo ni muda muafaka kwa sababu Hospitali ya Wilaya Handeni haikuwa na huduma hiyo kwa muda mrefu kitendo kilichokuwa kinapelekea baadhi ya Watoto njiti kupoteza maisha njiani wakiwa wanapelekwa kupata huduma hiyo kwenye hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Tanga ( Bombo) iliyopo umbali wa zaidi ya kilometa 150 kutoka Handeni Mji.
picha mbali mbali wakati wa tukio la makabidhiano ya vifaa kwa huduma ya Watoto njiti.
Barabara ya Korogwe - Handeni
Anuani ya Posta: S.L.P 51 HANDENI
Simu ya Mezani: 027-2641807
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: td@handenitc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.