Kamati ya Fedha na Utawala katika Halmashauri ya Mji Handeni imeridhishwa na kupongeza hatua ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Hayo yamejiri leo wakati ikifanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo iliyotekelezwa katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2018/2019.
Wajumbe wa Kamati hiyo wakiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe.Twaha Mgaya ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kwenjugo walijionea hatua za ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika Shule ya Msingi Lumbizi iliyopo Kata ya Kideleko ambapo kwa kiasi kikubwa vimekamilika, mradi ambao bali ya kutekelezwa na Serikali pia nguvu za Wananchi zimechangiwa.
Kukamilika kwa miundombinu hiyo ya kutasaidia kupunguza msongamano wa wanafunzi kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa na hivyo kutekeleza kwa ufanisi sera ya elimu bila malipo.
Vyumba viwili vya madarasa katika Shule ya Msingi Lumbizi mara baada ya kutembelewa na Kamati ya Fedha na Utawala.
Pia kamati hiyo ilitembelea miradi ya vikundi vya wanawake na Vijana katika Kata za Kwenjugo, Mdoe na Chanika ambapo Halmashauri kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii kwa kutumia mapato yake ya ndani inatoa mikopo ya riba nafuu kwa vikundi hivyo.
Katika Kata ya Kwenjugo Kamati ilitembelea kikundi cha Mshikamano kinachojishughulisha na shughuli utengenezaji wa bidhaa mbalimbali za mikono kama vile mikoba mikubwa na midogo ya akina mama, sabuni, kapeti ndogo za mlangoni na bidhaa nyingine kutokana na mahitaji ya mteja.Wakizungumza wakati wa ziara hiyo Wanakikundi hicho wamesema bado wanaendelea kutafuta soko la bidhaa zao nje na ndani ya Handeni ambapo kwa kuanzia tayari wamepata soko Mkoani Arusha ambapo wamepewa tenda ya kutengeneza kapeti ndogo za mlangoni mia mbili.
Baadhi ya bidhaa mbalimbali hapo juu zinazotengenezwa na kikundi cha Mshikamano kilichopo Kata ya Kwenjugo.
Katika kufuatilia kama fedha zinazotolewa na Serikali kwa walengwa Kaya maskini kwa ufadhili wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Kamati ilimtembelea mnufaika Mwanaidi mkazi wa Mtaa wa Kwedigongo katika Kata ya Kwenjugo.
Mlengwa huyo katika kumfuatilia ameonesha mafanikio kwa kuboresha makazi yake ambapo amejenga nyumba ya bati vilevile kupitia TASAF katika maeneo yao Mwanaidi amesema wameamua kuanzisha vikundi vya ujasiliamali ambapo kwa kuanzia wameanza na ufugaji wa mbuzi.
Bi Mwanaidi mlengwa wa Kaya maskini akieleza jambo mbele ya Kamati ya Fedha na Utawala wakati za ziara
Aidha, miradi mingine iliyotembelewa ni pamoja na ule wa Ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Shule ya Msingi tarajali Kwelale, Ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Halmashauri, kikundi cha vijana kinachojishughulisha na utengenezaji wa fenicha mbalimbali za majumbani kilichopo Kata ya Chanika pamoja na kikundi cha kina mama seuta kinachoshughulika na ufugaji wa Samaki pamoja na vitalu vya miti
Barabara ya Korogwe - Handeni
Anuani ya Posta: S.L.P 51 HANDENI
Simu ya Mezani: 027-2641807
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: td@handenitc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.