Waziri Mkuu mhe. Kassim Majaliwa amewataka wakuu wa Idara kutumia siku 4 kwenda kusikiliza kero za Wananchi na kuwaelimisha kila mmoja katika sekta yake namna ambavyo watakavyoweza kunufaika kupitia Idara yake.
Majaliwa ameyasema hayo Machi 3, 2020 katika Viwanja vya Shule ya Msingi Chanika wakati akiwa katika ziara ya ukaguzi wa miradi mbalimbali inayotekelezwa na uongozi wa awamu ya tano.
Akiongea na watumishi Waziri Mkuu, Majaliwa amewataka watumishi kufahamu wajibu wao kwa wananchi kwa kuwa wananchi ndio wakuu wao. Huku akiwataka kufuata miongozo, taratibu na kanuni kwa kufuata falsafa ya Mkuu wa Nchi.
Katika ziara hiyo amewakumbusha madiwani kuwa wanawajibu wa kusimamia shughuli zote na nini kifanyike katika Halmashauri, usalama wa mali na fedha kuwa salama huku akiwataka kukemea mtu yoyote ambae hafuati utaratibu wa Halmashauri hiyo kwa kuzingatia sheria za nchi na maelekezo ya serikali kuu. Aliongeza Waziri Mkuu.
Kuhusu changamoto zinazowakabili Wananchi wa Halmashauri ya Mji Handeni hasa sekta ya Afya, Maji, Elimu pamoja na miundombinu ya barabara Waziri Mkuu ameahidi Serikali changamoto hizo itaendelea kuzitatua moja baada jingine, kwa upande wa Afya tayari Serikali imepanga kuajiri madaktari 1000 ambapo wakati wa mgao Halmashauri ya Mji Handeni itapewa kipaumbele ,vile vile suala la vifaa tiba hasa X-ray italetwa tena ya kisasa.
Waziri Mkuu akiwahutubia Wananchi kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Chanika tarehe 03/03/2020.
Wananchi wakifuatilia hotuba ya Waziri Mkuu kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Chanika tarehe 03/03/2020.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe.Godwin Gondwe akiwahutubia Wananchi wakati wa ziara ya Waziri Mkuu.(picha kwa hisani ya Rajabu Athumani)
Barabara ya Korogwe - Handeni
Anuani ya Posta: S.L.P 51 HANDENI
Simu ya Mezani: 027-2641807
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: td@handenitc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.