Halmashauri ya Mji Handeni ni kati ya Halmashauri 11 zinazounda Mkoa wa Tanga. Halmashauri hii ilianzishwa kwa Tangazo la Serikali (GN) Namba 181 la tarehe 17 Juni 2011 na kuanza kazi rasmi Julai 2015 ikiwa na eneo lenye ukubwa wa Kilometa za Mraba 647.5 yenye Tarafa 1, Kata 12 na Mitaa 60. Halmashauri ya Mji Handeni ina jumla ya watu 108,968 (Wanaume 53,086, Wanawake 55,882) na Kaya 25,465, kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022.
Halmashauri ya Mji Handeni ipo kati ya nyuzi za Latitudo 4° 55’ na 6° 04’ Kusini na kati ya nyuzi za Longitudo 37° 47’ na 38° 46’ Mashariki mwa Meridiani Kuu ya Greenwich.
Makao Makuu ya Halmashauri ya Mji Handeni yapo katika Kata ya Kwenjugo Mtaa wa Ngugwini. Halmashauri ya Mji Handeni haina pwani na ipo katika kimo cha kati ya mita 600 hadi mita 1,000 kutoka usawa wa bahari.
Takribani asilimia 70 ya wakazi wa Halmashauri ya Mji Handeni wanajihusisha na shughuli za kilimo na ufugaji, asilimia 27 wanajishughulisha na biashara ndogo ndogo na ajira binafsi (maduka, wafanyabiashara, vibarua) na asilimia 3 wameajiriwa katika sekta za umma.
Halmashauri ina ukubwa wa Hekta 64,750 ambapo eneo linalofaa kwa kilimo na mazao mchanganyiko ni hekta 48,577.5. Mchanganuo wa maeneo mengine ni kama ifuatavyo;

Barabara ya Korogwe - Handeni
Anuani ya Posta: S.L.P 51 HANDENI
Simu ya Mezani: 027-2641807
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: td@handenitc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.