MAJUKUMU YA IDARA YA KILIMO,UMWAGILIAJI NA USHIRIKA.
1. Kuboresha Huduma za Ugani kwa wakulima katika Halmashauri ya Mji.
2. Kujenga na kuiendeleza Miundombinu ya Umwagiliajji
3. Kuendeleza matumizi sahihi ya pembejeo za kilimo kama vile mbolea, Matumizi ya mbegu bora na viuatilifu.
4. Kuendeleza matumizi ya zana bora za kilimo kwa kusaidia uwezeshaji wa matrekta makubwa na kuyasambaza kwa wakulima .
5. Kuanzisha mashamba darasa katika Kata zinazojishughulisha na Kilimo
6. Kuendeleza teknolojia za usindikaji na hifadhi ya mazao ili kuongeza thamani na kuboresha mfumo wa masoko .
7. Kuendeleza kilimo cha mazao ya biashara (Machungwa,Maembe na Katani)
8. Kuwawezesha Wakulima kushiriki maonesho ya nanenane ya kanda ya Mashariki.
9. Kuwezesha mpango wa matumizi bora ya Ardhi Mjini.
10. Kuhamasisha uanzishwaji wa vyama vya ushirika wa wakulima AMCOS na SACCOS.
11. Kutoa Elimu ya Ushirika kwa wanachama na wasio wanachama wa vyama vya ushirika.
12. Kuviunganisha vyama vya ushirika na wadau wengine( TAASISI ZA FEDHA Kuboresha afya ya Mifugo kwa kutoa kinga dhidi ya maradhi mbali mbali.
HUDUMA ZINAVYOPATIKANA.
• Kupata ushauri wa moja kwa moja toka Ofisi ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika katika Halmashauri.
• Kupata ushauri wa ana kwa ana toka kwa Wataalam wa Halmashauri, Kata au kwenye Mitaa katika shamba la Mkulima
• Kupata ushauri toka ofisi ya Kata au ya Mtaa.
• Mafunzo kwa njia ya Mikutano ( warsha na semina mbalimbali)
• Mafunzo kwa njia ya Vikundi.
Barabara ya Korogwe - Handeni
Anuani ya Posta: S.L.P 51 HANDENI
Simu ya Mezani: 027-2641807
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: td@handenitc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.