MAJUKUMU YA IDARA YA MAZINGIRA NA UDHIBITI WA TAKA NGUMU
1. Kufuatilia utekelezaji wa Sera na Sheria zinazohusiana na usimamizi wa Mazingira katika Halmashauri ya Mji Handeni
2. Kufuatilia na kuainisha maeneo yaliopo katika Halmashauri ya Mji Handeni ambayo yanapaswa kuhifadhiwa.
3. Kushiriki katika kuandaa Mpangokazi na Bajeti ya Idara ya Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu ya kila mwaka.
4. Kushiriki kuutekeleza Mpango kazi wa Idara ya Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu.
5. Kutoa Elimu ya Hifadhi ya Mazingira kwa Jamii na wadau wengine.
6. Kukusanya Takwimu na Taarifa mbalimbali zinazohusu usimamizi na hifadhi ya Mazingira katika Halmashauri ya Mji Handeni.
7. Kutoa ushauri kuhusu maeneo yaliyoathirka kutokana na shughuli za uchumi zisizo endelevu (Kama vile – Uchimbaji wa madini,Kilimo, Ujenzi, Ufugaji nk.)
8. Kushiriki katika kupanga na kusimamia zoezi zima la Usafi wa mazingira unaofanyika kila jumamosi ya mwisho ya kila mwezi.
Barabara ya Korogwe - Handeni
Anuani ya Posta: S.L.P 51 HANDENI
Simu ya Mezani: 027-2641807
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: td@handenitc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.