Kuratibu shughuli zote zinazohusu uchaguzi(uchaguzi wa serikali za Mitaa, uchaguzi mkuu na chaguzi ndogo zote zitakazo jitokeza baada ya uchaguzi kufanyika).
Kuratibu zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa uchaguzi mkuu na Orodha ya wapiga kura kwa Uchaguzi wa serikali za Mitaa.
Kuratibu masuala yote muhimu kwa ajili ya kuwezesha zoezi la uchaguzi (masuala hayo ni pamoja na maandalizi ya uteuzi wa wagombea, kuratibu kampeni za wagombea, maadalizi ya vituo vya kupigia kura, mafunzo kwa washiriki wote wa mazoezi ya uchaguzi. Mambo yote haya yanafanyika kwa ushiriki wa karibu na TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI na Wizara inayosimamia Uchaguzi wa serikali za Mitaa).
Kushirikiana na Idara ya Utumishi kuhakikisha mafunzo ya mara kwa mara yanafanyika kwa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa ili kuwawezesha kutekeleza majukumu yao kwa Mujibu wa Sheria.
Kumshauri Mkurugenzi juu ya masuala yote yahusuyo uchaguzi katika Halmashauri ili kuwezesha mazoezi hayo kufanyika kwa mujibu wa Sheria.
Kutekeleza majukumu mengineyo kwa maelekezo ya Mkurugenzi wa Halmashauri.