Kupanga na kusimamia utekelezaji wa Sera, Sheria na Waraka wa utoaji wa elimu ya Awali, Msingi, Sekondari, Mahitaji Maalum na elimu isiyo rasmi.
Kupanga upatikanaji, usambazaji na matumizi ya rasilimali katika shule za Msingi na Sekondari.
Kusimamia upimaji endelevu wa Mitihani ya Taifa katika shule za Msingi na Sekondari.
Kusimamia utoaji wa elimu ya watu wazima na elimu isiyo rasmi katika ngazi ya Awali, Msingi na Sekondari.
Kuratibu elimu ya stadi za maisha katika shule za Msingi na Sekondari.
Kufanya tathmini ya mahitaji maalum, elimu ya watu wazima na elimu isiyo rasmi.
Kutoa ushauri kuhusu uanzishaji na matengenezo ya vituo vya elimu ya watu wazima na visivyo rasmi.
Kusimamia utekelezaji wa Mipango na Programu za elimu ya msingi na sekondari.
Kuunda na kutunza kanzidata ya elimu ya Awali, Msingi na Sekondari
Kuratibu na kusimamia shughuli za michezo katika shule za Msingi na Sekondari.
Huduma ya Kilimo na Mifugo
Kukuza mabadiliko na maendeleo ya kilimo na mifugo.
Kuchambua, kutafsiri na kusimamia utekelezaji wa Sera, Sheria na udhibiti wa kilimo na Mifugo.
Kupendekeza viwango na bei za bidhaa na huduma zitokanazo na kilimo na mifugo.
Kuandaa mipango na programu fupi na ndefu za maendeleo ya kilimo na mifugo.
Kusimamia uendelezaji na utawala bora wa vyama vya ushirika katika Halmashauri.
Kutoa ushauri wa kitaalamu kwa wadau wanaohusika na kilimo na mifugo.
Kuandaa taarifa za kilimo na mifugo.
Kusimamia ukusanyaji na udhibiti wa mapato ya shughuli za kilimo na mifugo.
Huduma ya Maendeleo ya Jamii
Kusimamia shughuli za maendeleo ya jamii katika Halmashauri.
Kuchambua, kutafsiri na kusimamia utekelezaji wa Sera, Sheria na Taratibu zinazohusiana na maendeleo ya jamii.
Kuwezesha jamii kuanzisha, kupanga, kutekeleza na kutathmini programu na miradi yao wenyewe.
Kuandaa mipango na miradi ya muda mfupi na mrefu katika maendeleo ya jamii katika ngazi ya Halmashauri.
Kufanya utafiti na kupendekeza namna ya kushughulikia matatizo mbalimbali ya maendeleo ya jamii kwa kushirikiana na Wizara yenye dhamana na wadau wengine.
Kuratibu na kusimamia shughuli za watoa huduma wa Taasisi Ndogo za Fedha daraja la nne chini ya maelekezo ya Benki Kuu ya Tanzania (BOT).
Kuratibu na kusimamia shughuli za maendeleo ya kiuchumi kwa wanawake, watoto na watu wenye ulemavu.
Kuratibu utoaji wa mafunzo ya kuondoa umaskini, UKIMWI, dawa za kulevya na usawa wa kijinsia.
Kuratibu na kufuatilia shughuli za NGOs na CBOs katika maendeleo ya jamii.