MAJUKUMU YA IDARA YA MIPANGO TAKWIMU NA UFUATILIAJI
Mshauri wa Mkurugenzi mtendaji kuhusu masuala yote ya maendeleo ndani ya Halmashauri
Idara inaratibu na kuandaa taarifa mbalimbali za maendeleo ya Halmashauri
Idara inaratibu na kuandaa mpango wa bajeti wa Halmashauri
Idara inakusanya taarifa na takwimu mbali mbali za kiuchumi kwa ajili ya uchambuzi na uandaaji wa sera na mipango ya kiuchumi na kijamii Aidha idara inaandaa takwmu hizo na kuzichambua na kuzisambaza kwa wadau wote wa maendeleo
Idara inaratibu na kuanda taarifa za utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo zinazotekelezwa na idara na miradi mbalimbali ya kijamii
Idara inasimamia na kufanya tathmini ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya Halmashauri
Idara inaratibu shughuli za mfuko wa jimbo
Idara inatoa ushauri wa kitaalamu wa kuadika/kuandaa michanganuo ya miradi