Baraza la Madiwani Halmashauri ya Mji Handeni kwa muda wa siku mbili kuanzia tarehe 23-24/11/2017 limefanya mkutano wake wa kawaida kwa kipindi cha robo ya kwanza (Julai-Septemba) 2017/2018.
kwa Siku ya kwanza yaani tarehe 23/11/2017 Baraza lilipokea na kujadili taarifa mbalimbali za Maendeleo ngazi ya Kata kutoka kwenye Kata zote kumi na mbili (12) zinazounda Halmashauri ya Mji Handeni.Wakati wa kujadili taarifa za maendeleo ngazi ya Kata imeonyesha Wananchi wengi wakishirikishwa wanajitoa kushiriki shughuli za maendeleo ikiwemo kuchangia nguvu kazi kwenye miradi,Vilevile maeneo mengi ya Halmashauri ya Mji Handeni imeonyesha kuna chakula cha kutosha kutokana na msimu uliopita wananchi kupata mazao ya kutosha.
Siku ya pili Baraza la Madiwani lilipokea na kujadili taarifa za kamati zote zilizopo kwenye Halmashauri ya Mji kwa mujibu wa Sheria,wakati wa kupokea na kujadili taarifa za kamati mambo mawili makubwa yamejotokeza la kwanza migogoro ya Ardhi maeneo mbalimbali ya Halmashauri ya Mji,Pili uhaba wa watumishi unaoikabili Idara ya Afya.Kuhusu migogoro ya Ardhi Baraza limeazimia kuhakikisha linafuatilia kwa kina kila aina mgogoro na chanzo chake ili kuweza kujiridhisha kama ya kuchukua hatua,na kuhusu upungufu wa watumishia Idara ya Afya Baraza limeishukuru Serikali kwa kuweza kuipatia watumishi tisa (09) kwenye Ajira za hivi karibuni.
Akifunga mkutano wa Baraza hilo Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe.Twaha Mgaya amewaomba wajumbe kuendelea kuhimiza Wananchi kwenye maeneo yao kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuweza kujiletea Maendeleo.
Picha hapo juu zikionyesha wajumbe mbalimbali wakati wa mkutano wa Baraza la Madiwani Halmashauri ya Mji ukiendelea
Barabara ya Korogwe - Handeni
Anuani ya Posta: S.L.P 51 HANDENI
Simu ya Mezani: 027-2641807
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: td@handenitc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.