Baraza la Madiwani Halmashauri ya Mji Handeni limepokea na kujadili taarifa za utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo kutoka kwenye Kata kwa kipindi cha Robo ya Nne (April-June) kwa Mwaka wa fedha 2016/2017.Katika kupitia mambo mbalimbali yamejitokeza yanayohitaji kutiliwa mkazo ikiwemo kuelimisha Wananchi juu ya namna ya kujiletea maendeleo.
Katika kupitia taarifa hizo suala la mimba kwa wanafunzi wa kike limejitokeza huku takwimu zikionyesha kupungua kwa kasi tatizo hilo huku Baraza likipongeza juhudi zinazoonyeshwa na wadau mbalimbali wa maendeleo ili kuhakikisha kila mtoto anapata Elimu ili kuweza kuliletea Taifa maendeleo.Vilevile suala la Wananchi kushirikishwa kwenye shughuli za maendeleo limepongezwa sana kwa kutoa mifano,Wananchi wa Kata ya Msasa kwa nguvu zao wenyewe wamechonga barabara ambayo kwa sasa inawasaidia katika maeneo yao.
Mkurugenzi wa Halamshauri ya Mji Handeni Bw.Kenneth Haule kupitia Baraza hili amewaomba Wah.Madiwani wote kuhimiza suala la usafi katika maeneo yao,suala la Usafi limeonekana ni changamoto sana ambapo maeneo mengi hasa ya Kata za Mjini yaani Mdoe,Chanika na Vibaoni yana vichaka takataka zimezagaa,kwa kuanzia yeye mwenyewe Mkurugenzi aliwaita Ofisini kwake Watendaji wa Kata hizi na kujadili namna ya kutatua tatizo hilo.Ambapo kwa kuanzia Mwananchi yeyote atakayekaidi kufanya usafi kwenye eneo lake sheria itachukua mkondo wake.
Vilevile Mkurugenzi wa Halmshauri ya Mji amewataka Wenyekiti wa Serikali za Mitaa kuondoa tofauti zao ikiwemo mambo ya chuki,kuhujumiana na kutoaminiana kwa kuitisha mikutano ya Mitaa ili Wananchi wapate nafasi ya kuuliza na kupata ufumbuzi wa matatizo yao,kwa kutoitisha mikutano ya mitaa wanawanyima Wananchi fursa ya kuchangia mawazo yao namna ya kujiletea maendeleo.Amesema Wenyeviti wasioitisha mikutano ya Mitaa mamlaka zao ziwachukulie hatua kali za kisheria.
Baadhi ya Wahe.Madiwani wakipitia makabrasha wakati wa kupokea na kujadili taarifa za maendeleo ngazi ya Kata
Barabara ya Korogwe - Handeni
Anuani ya Posta: S.L.P 51 HANDENI
Simu ya Mezani: 027-2641807
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: td@handenitc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.