Katika kikao cha baraza la madiwani Halmashauri ya mji Handeni kilichofanyika tarehe 28-Oktoba 2022 katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Handeni, Makamu mwenyekiti Mh Hussein Khatibu (Diwani) amewasihi wataalamu wanaosimamia miradi mbalimbali ya serikali iliyoelekezwa kwenye Halmashauri ya mji Handeni kujijengea mazoea ya kuomba ushauri wa kitaalamu kwenye ngazi mbalimbali ikiwemo wilayani,mkoani hadi wizarani ili kuleta ufanisi na kupunguza migogoro katika utekelezaji wa miradi hiyo haraka iwezekanavyo .
Aidha katika kikao hicho, Katibu Tawala wa wilaya ya Handeni Mh.Mashaka Mgeta amewaelekeza wakuu wa idara, madiwani na viongozi mbalimbali wa kata, kila mmoja kwa nafasi yake kuwashauri wananchi kutumia vyema chakula kilichopo na kuhifadhi chakula hicho ipasavyo ili kujilinda na changamoto ya ukosefu wa chakula. Pia aliwaeleza kuwa hifadhi ya chakula iliyopo haijatupelekea kusema kuwa Halmashauri yetu ina njaa lakini kuchukua tahadhari ni muhimu.
Wakati huohuo katibu wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Handeni Mh.Anastazia Amasi amewataka madiwani kuwasisitiza wananchi juu ya utunzaji wa mazingira na kueleza kuwa uharibifu wa mazingira hupelekea hali ya janga la ukame na hivyo kusababisha njaa.
Barabara ya Korogwe - Handeni
Anuani ya Posta: S.L.P 51 HANDENI
Simu ya Mezani: 027-2641807
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: td@handenitc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.