Baraza la Madiwani katika Halmashauri ya Mji Handeni limekutana kwa ajili ya kuwasilisha na kupokea taarifa za utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya Kata zake mbalimbali.
Katika kikao hicho cha kujadili taarifa za robo ya tatu Januari hadi Machi kwa mwaka wa fedha 2017/2018, Mwenyekiti wa Halmashauri ,Twaha Mgaya ameipongeza Halmashauri ya Mji Handeni kwa kupata hati safi kutokana na ripoti ya Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali (CAG), Twaha ambaye ni Diwani wa Kata ya Kwenjugo aliwaomba madiwani waendelee kushikamana na kushirikiana na Wataalam wa Halmashauri ili waendelee kuwahudumia Wananchi katika Kata zao ili kuleta maendeleo katika Halmashauri ya Mji Handeni.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri Bw.Kenneth Haule amewaomba madiwani katika Kata zao washiriki kikamilifu kwenye miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo hayo ili utekelezaji wake uwe wa kiwango kinachokubarika ikiwa ni pamoja na kukamilika kwa wakati ."Waheshimiwa katika maeneo yenu kuna miradi mbalimbali ya maendeleo inatekelezwa lakini katika taarifa zilizowasilishwa hapa kutoka kwenye Kata zenu zijaona suala la miradi ya maendeleo likiripotiwa kwa kina ,mfano hatua ilipofikia,mipango endelevu kukamilisha baada ya Serikali kuchangia kiasi kikubwa cha fedha ",amesema
Mwenyekiti wa Halmashauri mhe.Twaha Mgaya akisoma sala ya kuiombea Halmashauri kabla ya kufungua Baraza
Wahe.Madiwani wakiuatilia mkutano wa Baraza
Wageni pamoja na wahe.Madiwani wakifuatilia mkutano wa Baraza wakati ukiendelea
Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia mkutano wa Baraza ukiendelea
Vilevile Baraza limepongeza wanafunzi wenye mahitaji maalum wanaosoma katika Shule ya Msingi Chanika walioshiriki mashindano ya michezo ya watu wenye mahitaji maalum ngazi ya Wilaya,Mkoa mpaka kitaifa kwa kufanikiwa kuiletea heshima Halmashauri ya Mji Handeni kwa kufanikiwa kunyakua medali kwenye michezo mbalimbali walioshiriki ikiwemo mpira wa miguu,pamoja na kukimbia, miongoni mwa medali zilizonyakuliwa na vijana hao ni pamoja na medali ya dhahabu.
Akizungumza kwenye Baraza hilo Mwl.Mkuu Shule ya Msingi Chanika wanaposoma vijana hao amesema" wanafunzi wenye mahitaji maalum kumbe na wao mwenyezi mungu amewajaalia vipaji mbalimbali ikiwemo michezo hivyo basi wakipewa nafasi wanafanya makubwa kama walivyofanya hawa ni vizuri kuendelea kuwawekea mazingira rafiki kulingana na mahitaji yao,naishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa Dkt John Magufuli kwa kuendelea kutuletea fedha za chakula kwa wanafunzi hawa".
Kwa upande wa Halmashauri wametoa zawadi mbalimbali kwa wanafunzi hao pamoja na walimu wao ikiwemo fedha tasilimu kwa kila mtu.
Mwl.Shule ya msingi Chanika akipokea zawdi kutoka kwa Mwenyekiti wa Halmashauri
Mwl.na kocha wa wanafunzi wenye mahitaji maalum akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa Halmashauri
Pichani hapo juu baadhi wanafunzi wenye mahitaji maalum walioshiriki michezo wakipokea zawadi zao
Barabara ya Korogwe - Handeni
Anuani ya Posta: S.L.P 51 HANDENI
Simu ya Mezani: 027-2641807
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: td@handenitc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.