Mkuu wa Wilaya ya Handeni Godwin Gondwe azindua rasmi Bodi mpya ya Mamlaka ya Maji na usafi na Mazingira mjini Handeni HUWASA ambayo imezinduliwa baada ya Mamlaka hiyo kukaa kwa kipindi cha muda mrefu bila kuwa na Bodi.
Mhe Gondwe akizindua bodi hiyo May 14, 2018 yenye Wajumbe saba (7) aliwaagiza wajumbe kuhakikisha wanashughulikia changamoto mbalimbali zinazoikabili Mamlaka ili huduma ya upatikanaji wa Maji kwa Wananchi wa Halmashauri ya Mji Handeni uwe wa asilimia 100.
Pamoja na kusistiza usimamizi wa upatikanaji wa maji kwa wateja Mkuu wa Wilaya Gondwe aliwaasa wajumbe wa Bodi mpya kuhaikikisha wanafanya kazi kwa weledi na kuisimamia Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira HUWASA ili iwe mojawapo ya Mamlaka zinazotaoa huduma nzuri nchini.
Wajumbe wa bodi mpya walioteuliwa ni Bw. Zakaria Killo (Mwenyekiti), Bw.Kenneth Haule (Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Handeni ), Bw. Mjinja Charles (Meneja wa Mamlaka ya Maji), mhe. Saleh Sebo (Mwakilishi wa Madiwani), Bw. Adam Msiraji (Mjumbe), Mwenjuma Mbega (mjumbe), Anna Mwagilo (mjumbe).
Akizungumza kwenye uzinduzi huo,Bw.Zakaria Killo (Mwenyekiti wa Bodi) amewaomba Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa Mji kuendelea kuwapa ushirikiano pale inapohitajika maana mamlaka inaonekana bado ina changamoto sana.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Handeni mhe.Twaha Ally Mgaya akizungumza kwenye uzinduzi wa Bodi ya HUWASA
Bw.Kenneth Haule Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji Handeni akizungumza kwenye uzinduzi wa HUWASA
DC Gondwe akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wageni waalikwa kwenye uzinduzi wa Bodi ya HUWASA
Barabara ya Korogwe - Handeni
Anuani ya Posta: S.L.P 51 HANDENI
Simu ya Mezani: 027-2641807
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: td@handenitc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.