Serikali kupitia mradi wa BOOST imetoa kiasi cha shilingi milioni 125.4 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa manne na matundu matatu ya vyoo, katika shule ya msingi Kwenjugo iliyopo katika mtaa wa Bwila kata ya Kwenjugo, akizungumza kwenye utambulishaji wa mradi huo kwa wananchi, Mwenyekiti wa BOOST Halmashauri ya Mji Handeni Mwl.Shomari Bane (Pichani), amewataka wananchi kushiriki katika ujenzi huo kwa moyo mmoja ili kuunga mkono jitihada za serikali katika kuendeleza miundombinu ya wanafunzi shuleni. Pia Mwl. Shomari Bane amewasisitiza viongozi wa shule na kamati ya ujenzi kuhakikisha kuwa mradi huo unakamilika kwa wakati kabla ya tarehe 20 Juni 2023.
Nae Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Kwenjugo Mwl.Omari Lumuli, ameishukuru serikali kwa kuwapelekea madarasa hayo manne pamoja na matundu matatu ya vyoo ambayo yanakuja kupunguza msongamano wa wanafunzi kwenye madarasa, hivyo kupelekea urahisi wa kufundisha kwa walimu na kusaidia wanafunzi hususani wenye ulemavu kuweza kupata huduma ya choo kwa urahisi.
Barabara ya Korogwe - Handeni
Anuani ya Posta: S.L.P 51 HANDENI
Simu ya Mezani: 027-2641807
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: td@handenitc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.