Serikali kupitia mradi wa BOOST imetoa kiasi cha shilingi milioni 56.3 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa mawili na matundu matatu ya vyoo katika shule ya msingi Mshikamano iliyopo katika mtaa wa Chang'ombe kata ya Chanika, akizungumza wakati wa utambulishaji wa mradi huo kwa wananchi, mratibu wa BOOST Halmashauri ya mji Handeni Bw. Sell Ngassa(Pichani) amewaambia wananchi mradi huu wa ujenzi ni wa kwao, hivyo ushiriki wao katika kila hatua ya ujenzi ni muhimu sana na unahitajika.
Nae Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Mshikamano Mwl. Beatrice Chayeka ameishukuru serikali kwa kuwapelekea madarasa hayo mawili kwakuwa yanaenda kupunguza msongamano wa wanafunzi madarasani kwenye shule yenye wanafunzi 898 na kuiomba serikali kuendelea kuitazama shule hiyo kwani bado inauhitaji wa miundombinu ya madarasa.
Barabara ya Korogwe - Handeni
Anuani ya Posta: S.L.P 51 HANDENI
Simu ya Mezani: 027-2641807
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: td@handenitc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.