Serikali kupitia mradi wa BOOST imetoa kiasi cha shilingi milioni 56.3 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa mawili na matundu matatu ya vyoo katika shule ya msingi Seuta iliyopo katika mtaa wa Bwawani, kata ya Mdoe. Akizungumza wakati wa utambulishaji wa mradi huo kwa wananchi Mratibu wa mradi wa BOOST Halmashauri ya Mji Handeni Mwl. Sell Ngassa (Pichani) amewasisitiza wazazi kutoa ushirikiano wa nguvu kazi ili kuunga mkono juhudi za serikali utakaopelekea kuongeza umoja na mshikamano baina ya wazazi, walimu, wanafunzi na serikali kwa ujumla.
Nae mwalimu mkuu wa shule ya msingi Seuta Mwl.Leonard Mndeme, ameishukuru serikali kwa kuwapelekea madarasa hayo mawili na mashimo matatu ya vyoo ambayo yanaenda kupunguza msongamano wa wanafunzi. Hivyo kuleta tija katika ufahamu na ufaulu kwa watoto pamoja na mazingira mazuri ya kujifunzia.
Barabara ya Korogwe - Handeni
Anuani ya Posta: S.L.P 51 HANDENI
Simu ya Mezani: 027-2641807
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: td@handenitc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.