Serikali kupitia mradi wa BOOST imeingiza kiasi cha shilingi milioni 540.3 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya msingi yenye mikondo miwili sawa na madarasa 16, matundu 18 ya vyoo na jengo la utawala, katika kata ya Mabanda, mtaa wa Mabanda.
Akizungumza wakati wa kuutambulisha mradi huo, Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Misima, Andrew Degeleki, ambaye shule yake ipo jirani na eneo linapokwenda kujengwa shule mpya, amesema anaishukuru serikali kwa uamuzi huo, kwani shule hiyo mpya ya mikondo miwili itapunguza mlundikano mkubwa wa wanafunzi darasani uliopo kwenye shule yake ambapo kwasasa shule yake ina wanafunzi 1937 na darasa lenye wanafunzi wachache lina wanafunzi 147, hali inayopelekea ufuatiliaji wa kitaaluma kwa mwanafunzi mmoja mmoja kuwa mgumu sana.
Barabara ya Korogwe - Handeni
Anuani ya Posta: S.L.P 51 HANDENI
Simu ya Mezani: 027-2641807
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: td@handenitc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.