Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Siriel Mchembe amewataka Wahe.Madiwani, Wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na Watendaji wa Kata kushirikiana na Ofisi yake katika kutekeleza ilani ya Uchaguzi ya chama tawala ili kuwaletea maendeleo Wananchi.
Amesema hayo leo Juni 23 alipokuwa akizungumza na viongozi hao katika kikao kazi cha kujitambulisha mara baada ya kuteuliwa hivi karibuni na Mhe Samia Suluhu Hassan kuwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni.
Alifafanua kuwa msingi wa maendeleo ya Taifa lolote unajengwa katika dhana ya umoja, msikamano, ushirikiano na mahusiano mazuri baina ya viongozi ambao ni watekelezaji wa Sera mbalimbali pamoja na wananchi wenyewe ambao ni wanufaika wa fursa za maendeleo zinazo letwa na serikali kupitia miradi mbalimbali.
Barabara ya Korogwe - Handeni
Anuani ya Posta: S.L.P 51 HANDENI
Simu ya Mezani: 027-2641807
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: td@handenitc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.