Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Wakili Albert Msando, amefanya ziara kutembelea maeneo yote ambayo mradi wa BOOST utatekelezwa. Mradi huo ni wa uboreshaji wa miundombinu ya elimu ya msingi ikiwamo ujenzi wa shule mpya, madarasa na matundu ya vyoo.
Mkuu wa Wilaya ameeleza kwamba,
“Simamieni hii miradi, wanakamati jadilianeni, fikieni muafaka katika kila hatua mnayopiga, msilumbane na kukwamisha mradi, ofisi yangu itawapeni na jeshi la akiba mlitumie kama nguvu kazi katika utekelezaji wa miradi hii, vitu vinavyoweza kupatikana kwenye maeneo yetu kama maji, mchanga tuvitumie hivyo ili kupunguza gharama, fedha mtakazoweza kuziokoa zikatusaidie kwenye ukarabati wa miundombinu chakavu na ile ambayo sio toshelezi kwenye shule zetu, sitakubali uzembe kwenye fedha hizi"
Mh. Albert Msando, akiwa ameambatana na wajumbe wa kamati ya BOOST Halmashauri ya Mji Handeni alitembelea mradi wa ujenzi wa shule mpya ya msingi yenye mikondo miwili katika kata ya Mdoe, mradi wa ujenzi wa shule mpya ya msingi yenye mikondo miwili katika kata ya Mabanda na mradi wa ujenzi wa madarasa manne na matundu matatu ya vyoo katika Kata ya Kweinjugo, shule ya msingi Kweinjugo iliyopo kata ya Kwenjugo. Miradi hiyo yote mitatu aliyotembelea imepatiwa jumla ya shilingi Bilioni moja milioni mia mbili na sita kutoka serikali kuu kupitia mradi wa BOOST.
Barabara ya Korogwe - Handeni
Anuani ya Posta: S.L.P 51 HANDENI
Simu ya Mezani: 027-2641807
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: td@handenitc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.