Halmashauri ya Mji Handeni kwa kushirikiana na Kampuni ya Dar es salaam M/S MACDONALD CIVIL ENGINEERING AND BUILDING CONSTRACTOR wameweka makubaliano kwa kutia saini kuanza ujenzi wa miundombinu ya Maji kutoka Kata ya Kwenjugo mpaka Kata ya Malezi.
Mradi huo unatarajia kugharimu Tshs.milioni 518,532,710 na kwamba unatarajiwa kujengwa ndani ya miezi 6.
Akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba huo,Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Handeni Mhe.Twaha Ally Mgaya amesema lengo ni kuhakikisha Wananchi wa Kata ya Malezi na maeneo yote ambapo mradi umekusudiwa kupita na kutoa huduma ya Maji wananufaika kwa kupata Maji ya uhakika na si vinginevyo,Vile vile amemtaka mkandarasi kuhakikiksha anakamilisha mradi kwa wakati kutokana na mkataba unavyotaka ili kuwanusuru Wananchi na kero ya ukosefu wa Maji ya Uhakika kwa kipindi cha muda mrefu.Mhe Mwenyekiti pia amemshauri mkandarasi kuhakikisha anakuwa karibu wakati wa utekelezaji wa mradi huo ili kuepuka dosari mbalimbali zinazoweza kujitokeza kuliko kuwategemea wasaidizi wake kaswa kiasi kikubwa ambapo uzoefu unaonyesha mara nying wasidizi wengi siyo waaminifu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Handeni Bw.Kenneth Haule amemtaka mkandarasi kutambua kwamba Wananchi wa Kata ya Malezi wana shauku kubwa na mradi huo na matarajio yao makubwa ni kuona mradi huo unawakomboa kutoka kwenye kero ya muda mrefu ya ukosefu wa Maji ya uhakika,Hivyo basi mkandarasi ni lazima atekeleze mradi kwa viwango vinavyokubalika kutokana na mkataba na kuhakikisha mradi ukikamilika Wananchi wanapata Maji,Bila mradi kutoa Maji baada ya kukamilika itakuwa aina maana hata ajenge miundombinu mizuri ya namna gani.
Akizungumzia mradi huo Kaimu Mkuu wa Idara ya Maji Halmashauri ya Mji Handeni Mhandisi Dismas Kway amesema usanifu wa mradi huo ulifanyika kwa kushirikiana na Wataalam kutoka Wizara ya Maji ambapo walijiridhisha kwamba mradi huo utakaokuwa una jumla ya vituo 15 vya kutolea huduma ukikamilika utaleta tija kwa wananchi na wakazi ya Kata ya Malezi kwa kiasi kikubwa.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Handeni Mhe.Twaha Ally Mgaya kwenye hafla ya kusain mkataba
Bw.Richard Unambwe (katikati) Mwanasheria wa Halmashauri ya Mji Handeni akifafanua jambo kwenye mkataba
Mwakilishi wa Kampuni ya MACDONALD (mwenye kofia) akifuatilia mjadala wakati wa hafla hiyo
Barabara ya Korogwe - Handeni
Anuani ya Posta: S.L.P 51 HANDENI
Simu ya Mezani: 027-2641807
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: td@handenitc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.