Kutokana na utafiti uliofanyika katika Wilaya ya Handeni kuhusu zao la korosho na kuonekana linaweza kustawi vizuri Halmashauri imeendelea na zoezi la kuhamasisha wakulima kupanda zao hilo kwa wingi.Katika kuhamasisha upandaji wa korosho kwa wakulima Halmashauri imegawa miche ya korosho bila malipo kwa Wakulima.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wakati wa zoezi hilo Kaimu Mkuu wa Idara ya Kilimo Bw.Leopold Ngowi amesema jumla ya miche 7500 imepokelewa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe na itagawiwa kwa Wakulima wote watakaojitokeza kulingana na idadi ya miche iliyopo.
Jumla ya miche 5000 iligawiwa kwa wakulima ambapo mpaka sasa mikorosho 1600 imestawi kwenye maeneo mbalimbali,hivyo basi ushauri unatolewa kwa wakulima kutilia maanani zao la korosho maana mbeleni litakuwa zao la biashara na kuinua wakulima kiuchumi kama yalivyo mazao mengine kama mahindi,mbaazi,mihogo inayolimwa kwa wingi wilayani Handeni.
pichani Wakulima wakichagua mikorosho
Barabara ya Korogwe - Handeni
Anuani ya Posta: S.L.P 51 HANDENI
Simu ya Mezani: 027-2641807
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: td@handenitc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.