Kamati ya Fedha na Uongozi ya Halmashauri ya Mji Handeni imefanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 1.2 katika robo ya pili ya mwaka wa fedha 2024/2025. Ziara hiyo imelenga kufuatilia utekelezaji wa miradi hiyo, kuhakikisha matumizi sahihi ya rasilimali, na kuimarisha uwajibikaji wa watendaji kwa manufaa ya wananchi wa Handeni.
Katika ziara hiyo, Kamati ilikagua miradi sita ya kimkakati ambayo ni:Ujenzi wa Madarasa Mawili katika Shule ya Msingi Msasa, uliogharimu Shilingi Milioni 50. Ujenzi wa Zahanati ya Msasa, yenye thamani ya Shilingi Milioni 102.1. Ujenzi wa Nyumba Nne za Wakuu wa Idara, wenye thamani ya Shilingi Milioni 320.Ujenzi wa Mabweni Mawili katika Shule ya Sekondari Misima, unaofadhiliwa na Kampuni ya Barrick, wenye thamani ya Shilingi Milioni 260.Mradi wa Land Scape katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Handeni, wenye thamani ya Shilingi Milioni 379.Ziara hiyo iliongozwa na Mkurugenzi wa Halmashauri, Bi. Maryam A. Ukwaju, akishirikiana na Mwenyekiti wa Halmashauri, Mhe. Mussa Mkombati, pamoja na Wakuu wa Idara na Watendaji wa Vitengo mbalimbali.Akizungumza baada ya ukaguzi huo, Mhe. Mussa Mkombati alitoa shukrani za dhati kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuhakikisha upatikanaji wa fedha za utekelezaji wa miradi hiyo. Aidha, aliwashukuru wafadhili, wakiwemo Kampuni ya Barrick, kwa kuchangia maendeleo ya wananchi wa Handeni. Mjini, Alisisitiza umuhimu wa uwajibikaji zaidi kutoka kwa watendaji ili kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati na kwa viwango bora vinavyostahili.Miradi hii inatarajiwa kuleta manufaa makubwa katika sekta za elimu, afya, na makazi, pamoja na kuboresha mazingira ya kazi kwa watumishi wa umma. Hii itachochea maendeleo endelevu na kuboresha ustawi wa jamii katika Halmashauri ya Mji Handeni.
Barabara ya Korogwe - Handeni
Anuani ya Posta: S.L.P 51 HANDENI
Simu ya Mezani: 027-2641807
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: td@handenitc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.