Kamati ya Fedha na Uongozi ya Halmashauri ya Mji Handeni imefanya ziara ya kikazi kwa kutembelea miradi mbalimbali ya Maendeleo.
Ziara hiyo imeongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri mhe.Twaha Ally Mgaya imezuru katika miradi hiyo kwa lengo la kujionea hali halisi ya shughuli mbalimbali zinazoendelea ikiwemo Ujenzi.
Miongoni mwa miradi iliyotembelewa na kamati hiyo ni kuona ujenzi wa mradi wa Maji Kata ya Malezi ambapo kwa asilimia kubwa ya mradi huo umekamilika baada ya kamati kushuhudia baadhi ya Wananchi wa Malezi wakipata huduma ya Maji kutoka kwenye mradi huo ikiwa na hatua za majaribio.Vile vile kamati imetembelea mradi wa Ujenzi wa Jengo la Ofisi la Halmashauri ya Mji ambapo mkandarasi wa mradi huo Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) wamesisitiza kukamilisha mradi huo kwa wakati.
Miradi mingine ni kuona hali halisi ya ujenzi wa maabara ya Sayansi Shule ya Sekondari Kileleni,sawia na ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Shule ya Msingi Kweinjugo,Pongwe na Lumbizi.Vile vile kamati imetembelea eneo la ujenzi wa Zahanati ya Msaje.
Wananchi wa Malezi wakipata huduma ya Maji Wakati kamati ya Fedha na Uongozi ilipofanya ziara kwenye eneo la mradi.
Mkurugenzi wa Halmashauri bw.Kenneth K.Haule akifafanua jambo mbele ya kamati ya Fedha na Uongozi wakati wa ziara
Tenki kubwa la kuhifadhia Maji lililojengwa kwenye mradi wa Maji Malezi.
Ujenzi wa jengo la Ofisi ya Halmashauri ya Mji Handeni ukiendelea
Mwl.Mkuu msaidizi wa Shule ya Msingi Pongwe Bi.Fatuma akisoma taarifa ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa mbele ya wajumbe wa kamati ya Fedha
Barabara ya Korogwe - Handeni
Anuani ya Posta: S.L.P 51 HANDENI
Simu ya Mezani: 027-2641807
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: td@handenitc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.