Kamati ya fedha na uongozi ya Halmashauri ya Mji Handeni mnamo tarehe 15 -16/08/2019 imefanya ziara ya kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa.
Ziara hiyo imeongozwa na Mwenyekiti ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri mhe.Twaha Ally Mgaya.katika ziara hiyo kamati ilishiriki na Wananchi wa Kata ya Malezi kwenye zoezi la kuchimba msingi kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Sekondari katika eneo hilo.
Vile vile kamati ilitembelea ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule za msingi tarajali Kwelale ambapo chumba kimoja cha darasa na Ofisi ya walimu vimekamilika, mpakani ambapo vyumba viwili vimekamilika kamati iliruhusu vianze kutumika ili kupunguza changamoto ya umbali kwa wanafunzi ambao wanasoma shule msingi Kwediyamba.
Kamati pia ilitembelea mradi wa kiwanda cha uzalishaji chaki kutoka kwa kikundi cha CAMA kikundi hiki kinafadhiliwa na CAMFED ambapo pia Halmashauri imetoa mchango wake kuhakikisha vijana hao wanapata soko la chaki wanazozalisha kupitia Shule za msingi na Sekondari.
Wananchi wa Kata ya Malezi wakichimba msingi kwa ajili ya ujenzi wa shule ya Sekondari Malezi .
Muonekano wa chumba cha darasa na Ofisi ya Walimu katika shule ya msingi tarajali Kwelale vimekamilika tayari kwa matumizi
Muonekano wa matundu ya vyoo katika shule ya msingi Kiseriani yakiwa tayari yameanza kutumika
Kiwanda cha kuzalisha chaki cha kikundi cha CAMA kilichopo mitaa ya bomani kilipotembelewa na kamati ya fedha.
Wajumbe wa kamati ya fedha na uongozi wakipokea taarifa katika Shule ya msingi tarajali kwelale wakati wa ziara.
Barabara ya Korogwe - Handeni
Anuani ya Posta: S.L.P 51 HANDENI
Simu ya Mezani: 027-2641807
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: td@handenitc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.