Kamati ya fedha na utawala kwa kuambatana na wataalam mbalimbali kutoka Halmashauri ya Mji Handeni wamefanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kwa lengo la kujua hali halisi ya miradi,Mahali ilipofika na thamani ya pesa iliyotumika (value for money).
Maeneo yaliyotembelewa na Kamati ya fedha na utawala ni pamoja na eneo la ujenzi wa Ofisi mpya za Halmashauri ya Mji Handeni,Ujenzi wa matundu ya vyoo katika Shule za Msingi Antakae,Misima na Kwakivesa,Ujenzi wa mabweni mawili (2) na vyumba viwili (2) vya madarasa katika Shule ya Sekondari Handeni,Ujenzi wa choo soko jipya la Seuta,Kikundi cha vijana cha deep c furniture kilichopo Kata ya Mabanda,na walengwa/wanufaika wa mradi wa TASAF ambapo kaya mbili (2) zilitembelewa.
Katika ziara hizo Waheshimiwa Madiwani wamefanikiwa kupata maelezo ya lini ujenzi wa Ofisi mpya za Halmashauri ya Mji Handeni litaanza kujengwa,na namna ambavyo Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ambao ndiyo wanahusika na ujenzi huo namna walivyojipanga kuhakikisha mradi huo unaenda kwa kasi inayotakiwa pamoja na ubora.
Aidha Kamati imepongeza ya ujenzi wa matundu ya vyoo katika Shule ya Msingi Kwakivesa kwa kazi nzuri waliyoifanya kwa kuhakikisha fedha waliyoipata inatumika ipasavyo kwa kuonyesha kazi imefanyika kwa kiwango kikubwa vilevile na nguvu kazi ya wanajamii imechangia kwa kiasi kikubwa mradi huo kwenda kwa kasi.
Vilvile Kamati ya fedha na utawala imepongeza kikundi cha vijana cha deep c furniture kilichopo Kata ya Mabanda kwa kundelea kuwa wabunifu kwa kutengeneza bidhaa mbalimbali zenye ubora na kukuza Soko lao ndani na nje ya Halmashauri ya Mji Handeni,Kikundi hiki kinatengeneza bidhaa kama majiko yenye ukubwa tofauti tofauti,Ovena za kuokea mikate na kuchoma nyama,na matranka kwa ajili ya wanafunzi.
Kwenye miradi ambayo Wananchi wanapaswa kushiriki nguvu kazi Kamati imeagiza viongozi wa Kata na Mitaa maeneo husika kuhakikisha wanahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki kazi ambazo wanaweza kufanya ili kusaidia ukamilishwaji wa miradi kwa wakati,hasa ukizingatia miradi hiyo ni kwa ajili ya manufaa yao na jamii nzima inayozunguka eneo husika,hivyo wanaowajibu kuhakikisha wanashiriki kikamilifu na kumiliki mradi uliopo kwenye maeneo yao ili uweze kutunzwa vyema na wananchi wenyewe.
picha hapo juu zikionyesha wajumbe wakikagua na kupata maelezo kwenye eneo la ujenzi wa Ofisi mpya za Halmashauri
Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe.Twaha Mgaya akishiriki zoezi la ujenzi wa matundu ya vyoo Shule ya Msingi Misima
Barabara ya Korogwe - Handeni
Anuani ya Posta: S.L.P 51 HANDENI
Simu ya Mezani: 027-2641807
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: td@handenitc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.