Mei 8,2018 siku ya Jumanne Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Handeni mhe Twaha Ally Mgaya ameiongoza kamati ya kudumu ya Fedha na Utawala ya Baraza la Madiwani kutembelea maeneo ya utekelezaji wa miradi yaliyopo Halmashauri ya Mji Handeni.
Katika ziara hiyo,mhe Twaha aliongozana na Madiwani ambao ni wajumbe wa kamati ya fedha na utawala pamoja na wataalam wa Idara na Vitengo mbalimbali.Maeneo ya miradi yaliyotembelewa na kamati hiyo ni eneo la ujenzi wa jengo la Ofisi ya Halmashauri,shamba darasa lililopo Shule ya Msingi Ngugwini,Mradi wa Maji Malezi.
Akizungumza katika ziara hiyo eneo la ujenzi wa jengo la Ofisi ya Halmashauri,mhe Twaha amewasisitizia Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) wanaojenga jengo hilo kuzidi kuongeza kasi ya ujenzi maana jengo hilo linasubiriwa kwa hamu kubwa kutokana na ufinyu wa Ofisi zinazotumika kwa sasa na Halmashauri ambayo imekuwa ni changamoto kwa Watumishi,kwa upande wao TBA wamesema wapo tayari na wanazidi kujipanga ipasavyo kuhakikisha jengo hilo linakamilika kwa wakati ikiwezekana kukamilisha kabla ya mkataba unavyosema.
Vilevile kamati ikiwa kwenye eneo la shamba darasa katika Shule ya Msingi Ngugwin imepongeza uongozi wa Shule kwa kuwa wabunifu na kuwashirikisha wanafunzi kwenye uandaaji wa shamba hilo jambo litakalopelekea wanafunzi hao kupeleka ujuzi huo kwa wazazi wao ili kuondoa dhana ya kilimo kisichofuata kanuni ili kuweza kuongeza mavuno kwa misimu ijayo ya kilimo.
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa jengo la Ofisi ya Halmashauri
Barabara ya Korogwe - Handeni
Anuani ya Posta: S.L.P 51 HANDENI
Simu ya Mezani: 027-2641807
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: td@handenitc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.