Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndg.Charles Kabeho ameipongeza Halmashauri ya Mji Handeni kwa kuanzisha mfumo wa taarifa za Wagonjwa hospitali (GoT-HoMIS) kwenye Hospitali ya Wilaya Handeni..
Ameyasema hayo leo tarehe 08/10/2018 wakati akifungua mfumo huo ikiwa ni miongoni mwa miradi aliyotembelea kwenye mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa kwenye Halmashauri ya Mji Handeni,Kiongozi huyo amezishauri Halmashauri nyingine Nchini kuiga mfano kwa kuanzisha mfumo huo ili kuboresha huduma za Afya kwani utapunguza adha kwa Wagonjwa vile vile mfumo huo unatarajia kuongeza mapato ya hospitali.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndg.Charles Kabeho akisalimiana na Wagonjwa
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Ndg.Charles Kabeho akifungua mfumo wa Hospitali (GoT-HoMIS)
Barabara ya Korogwe - Handeni
Anuani ya Posta: S.L.P 51 HANDENI
Simu ya Mezani: 027-2641807
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: td@handenitc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.