Leo Jumatatu tarehe 24/04/2023 Halmashauri ya Mji Handeni imefanya zoezi la usafi wa mazingira Kuelekea kilele cha maadhimisho ya 59 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, wenye kauli mbiu “Umoja na mshikamano ndio nguzo ya kukuza uchumi wetu”, katika maeneo mbalimbali yanayozunguka makazi ya watu, maeneo ya kutolea huduma ikiwemo Hospitali ya Halmashauri ya Mji Handeni na maeneo ya biashara. Viongozi, watumishi na wananchi kwa ujumla wamejumuika katika zoezi hilo.
Watumishi wa Halmashauri ya Mji Handeni, wakifanya usafi wa mazingira katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji Handeni
Akizungumza na waliohudhuria zoezi hilo Afisa Afya wa Halmashauri ya Mji Handeni Ndugu.Jonas Mkondya, amewasisitiza wakazi wa Halmashauri ya Mji Handeni, kuhakikisha kuwa wanaweka mazingira safi na kusambaratisha mazalia yote ya mbu kwa kufyeka nyasi, kusambaratisha madimbwi, kuondoa chupa zilizowazi na vyombo vyote vinavyotumika kuhifadhia maji vifunikwe ili kudhibiti mazalia ya mbu na hatari ya kupata ugonjwa wa malaria hususani katika kipindi hiki cha mvua.
Nae mganga mkuu wa Halmashauri ya Mji Handeni Dokta.Feisal Said, ameishukuru ofisi ya mkuu wa wilaya kwa kujumuika pamoja katika zoezi la usafi lililofanyika kataka hospitali ya wilaya ya Handeni, pia amewasisitiza wakazi wote wa Halmashauri ya Mji Handeni kufanya zoezi la usafi kuwa ni endelevu kwa siku zote.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Handeni Ndugu.Gerald Kauki akiongea na watumishi waliojumukia katika usafi uliofanyika Hospitali ya Halmashauri ya Mji Handeni
Kaimu Mkurugenzi amewataka wananchi kuhakikisha kuwa wanatunza mazingira kwa kufanya usafi, kupanda miti kwa wingi katika kipindi hiki cha mvua na kuepuka ukataji hovyo wa miti, pia Ndugu.Gerald Kauki amewashukuru watumishi wote waliojumuika katika usafi huo kwani wameendelea kutoa ushirikiano katika shughuli mbalimbali za kijamii na kuwasihi kuendelea na mshikamano huo, kama ilivyo katika kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya muungano wa Tanganika na Zanzibar “Umoja na mshikamano ndio nguzo ya kukuza uchumi wetu”.
Barabara ya Korogwe - Handeni
Anuani ya Posta: S.L.P 51 HANDENI
Simu ya Mezani: 027-2641807
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: td@handenitc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.