Maadhimisho ya Juma la Elimu Mkoa wa Tanga yamefanyika kwa muda wa siku mbili kuanzia tarehe 26-27/04/2019 katika Wilaya ya Handeni.Katika maadhimisho hayo wadau mbali mbali wa Elimu wa Mkoa wa Tanga Wakiongozwa na Mhe.Martine Shigela (Mkuu wa Mkoa wa Tanga) walipata fursa ya kutembelea miradi ya Elimu ikihusisha Ujenzi wa vyumba vya madarasa, maabara, mabweni pamoja na shamba la Shule la takribani ekari ishirini lenye mazao mbali mbali ya chakula na biashara.
Mh. Shigela alipotembela shamba la shule ya Sekondari ya Komnyang’anyo lenye ekari zaidi ya 20 iliyopandwa mihogo, mahindi na korosho aliagiza kila Halmashauri kuiga mfano huo ili kuondokana na uhaba wa chakula shuleni kwani upatikanaji wa chakula una uhusiano mkubwa katika ufaulu wa wanafunzi.
Katika kikao cha tathmini ya maendeleo ya Elimu ya Mkoa Mh.Shigela alitaka kila ngazi ya Uongozi katika kila Halmashauri kufanya tatmini ya Elimu kila mara ili kujua changamoto za maendeleo ya Elimu mapema na kuzitatua kwa wakati ikiwemo suala la upatikanaji wa chakula shuleni, utoro wa wanafunzi, suala la mimba kwa wanafunzi na maendeleo ya taaluma na michezo.
Katika Maadhimisho hayo Mhe.Shigela aligawa zawadi kwa Shule, Wanafunzi pamoja na Walimu waliofanya vizuri kwenye sekta mbali mbali za Elimu.
RC Shigela akiwa na Wadau wa Elimu kwenye Shamba la Shule ya Sekondari Komnyang'anyo kwenye maadhimisho ya Juma la Elimu.
Mhe.Twaha Mgaya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Handeni akishiriki Shughuli ya Ujenzi kwenye Maadhimisho ya Juma la Elimu.
Bw.Kenneth Haule Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji handeni akiwasilisha taarifa ya tathimini ya Elimu katika maadhimisho ya Juma la Elimu
Barabara ya Korogwe - Handeni
Anuani ya Posta: S.L.P 51 HANDENI
Simu ya Mezani: 027-2641807
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: td@handenitc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.