Leo tarehe 13-12-2022 katika ukumbi wa Halmashauri ya mji Handeni zaidi ya makarani 12 wa uchaguzi mdogo wa udiwani wa Kata ya Vibaoni, Halmashauri ya Mji Handeni wamepatiwa mafunzo na maafisa wa Tume ya Taifa ya uchaguzi sambamba na kula kiapo mbele ya Hakimu Mkazi wa mahakama ya Wilaya ya Handeni Mh.Joakim Joram Mwakyolo
Hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya ya Handeni Mh.Joakim Joram Mwakyolo akithibitisha fomu za viapo vya makarani wa uchaguzi mara baada ya kula kiapo.
Akizungumza na Makarani waongozaji hao katika ufunguzi wa mafunzo hayo mara baada ya kula kiapo, Msimamizi Msaidizi Uchaguzi wa jimbo la Handeni Mjini Ndugu. Steven C. Bavu amewaasa Makarani waongozaji wapiga kura hao kuzingatia lugha nzuri, busara na hekima katika muda wote watakaotumika kutoa huduma kwa wapiga kura ili kufanikisha zoezi hilo kwenda vizuri mpaka mwisho.
Makarani wa uchaguzi mdogo wa kata ya Vibaoni wakiendelea kupatiwa mafunzo na maafisa kutoka Tume ya Taifa ya uchaguzi(NEC) katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Handeni
Uchaguzi mdogo wa kata ya Vibaoni unaotarajiwa kufanyika jumamosi tarehe 17-12-2022 unakuja kufuatia aliyekuwa diwani wa kata hiyo Ndugu.Ramadhani Kuyugu (CCM) kujiuzulu nafasi hiyo mara baada ya kupata ajira ya kudumu serikalini na hivyo kiti cha udiwani kata ya vibaoni kuwa wazi.
Nae Afisa kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bi.Margareth Chambiri pamoja na mambo mengine, amewataka makarani hao kuwapa kipaumbele watu wenye makundi maalumu watakaojitokeza kupiga kura kwa kutokukaa kwenye foleni bali wawazingatie na kuhakikisha wanapiga kura haraka na kuendelea na shughuli zao nyingine, akitolea mfano wa makundi hayo maalum ameyataja kuwa ni mama wajawazito, wenye watoto wachanga, watu wenye ulemavu wa viungo, wazee nk
Mgeni rasmi katika mafunzo ya siku moja ya makarani waongozaji wapigaji kura Bi. Margareth Chambiri akifunga mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Handeni
Picha ya pamoja ya makarani waongozaji na Mgeni rasmi mara baada ya kuhitimisha mafunzo ya siku moja
Abdulkadir Kassim
Handeni Mji
Barabara ya Korogwe - Handeni
Anuani ya Posta: S.L.P 51 HANDENI
Simu ya Mezani: 027-2641807
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: td@handenitc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.