Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Handeni, Mh. Mussa Abeid Mkombati(DIWANI), Leo Ijumaa tarehe 5/5/2023 ameendelea na ziara yake katika nyumba za ibada, kwa kuutembelea msikiti wa Kidato uliopo Mtaa wa Kwamngumi, Handeni Mjini.
Mh. Mkombati anafanya ziara hiyo ikiwa na lengo kuu la kuwaomba viongozi wa dini na waumini wa dini zote, kuliombea taifa dhidi ya ukatili kwa watoto na mapenzi ya jinsia moja.
"Watu wanaohamasisha matendo haya ni watu wenye fedha nyingi, sisi tumeamua kukimbilia kwa Mwenyezi Mungu atusaidie kutuepusha na kadhia hii, niwaombe sana mashekhe na waumini kwa ujumla, kuliombea taifa hili liweze kuepushwa na jambo hili" alisema.
Wiki iliyopita, Mh. Mkombati alitembelea jumla ya makanisa saba yanayoabudu siku ya jumapili yaliyopo Handeni Mjini na kesho ataendelea na ziara yake kwenye makanisa yanayoabudu Jumamosi.
Abdulkadir Kassim
Handeni Mji
Barabara ya Korogwe - Handeni
Anuani ya Posta: S.L.P 51 HANDENI
Simu ya Mezani: 027-2641807
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: td@handenitc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.