Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Handeni Mji Mh.Mussa Abeid Mkombati wakati akifungua kikao cha Baraza la Madiwani leo tarehe 28-04-2023.
"Nitumie fursa hii kukupongeza sana Mkurugenzi Bi.Maryam Ukwaju, mpaka mwezi machi ulishafikia 78% ya ukusanyaji mapato na kuipelekea Halmashauri kuongoza kimkoa,umepeleka fedha za mapato ya ndani kwenye miradi ya maendeleo kama inavyotakiwa na sasa tumepata hati safi, natambua usimamizi wako wa karibu kwa watumishi wako, kasi kubwa ya ukusanyaji mapato, ndio sababu ya haya yote. Hongera sana" alisema.
Kuhusu fedha zilizotolewa na serikali kuu kupitia mradi wa BOOST kiasi cha shilingi Bilioni moja, milioni mia nne hamsini na sita na laki mbili pamoja na fedha kiasi cha shilingi milioni mia tisa kwa ajili ya ujenzi wa jengo la dharura(EMD) na ukarabati wa hospitali ya wilaya ya Handeni, Mh.Mkombati alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwathamini wananchi wa Handeni Mji.
Aidha alitumia fursa hiyo kumpongeza Mkuu wa wilaya ya Handeni Mh. Albert Msando kwa kufanyia kazi kero za wananchi kwa wakati, akitolea mfano kupokea na kulifanyia kazi ombi la waheshimiwa madiwani la kuwekewa matuta barabarani ili kupunguza ajali za kugongwa kwa wanafunzi wanaosoma shule za msingi Chanika na Mshikamano.
Akizungumzia kuhusu suala la ukatili kwa watoto na mapenzi ya jinsia moja, Mh. Mkombati amelaani vikali vitendo hivyo vya mmomonyoko wa maadili katika jamii na kuwaomba viongozi wa dini kufanya maombi ya kitaifa kuliombea Taifa hili kama ambavyo wamekuwa wakifanya yanapotokea majanga ya corona ili kulinusuru taifa na changamoto ambayo inakwenda kuliondolea nguvu kazi za vijana.
Nae Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Handeni Bi. Maryam Ukwaju amemtaka kila mtu kwa nafasi yake kule aliko katika jamii tunazoishi kukemea vitendo hivi vya mmonyoko wa maadili, wananchi washiriki katika maelezi ya watoto, wasiwaache watoto bila uangalizi
"Tuwe sehemu ya kutoa elimu katika maeneo tuliyopo, mikutano ya hadhara, mikutano ya kata, popote pale tukatoe elimu kuhusu maadili na malezi ya watoto" alisisitiza.
Barabara ya Korogwe - Handeni
Anuani ya Posta: S.L.P 51 HANDENI
Simu ya Mezani: 027-2641807
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: td@handenitc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.