Mkuu wa mkoa wa Tanga Mh. Waziri Kindamba amesema anataka kuona viongozi wa chama na serikali katika mkoa wa Tanga wanafanya kazi kwa ushirikiano, upendo na mshikamano ili wasimuangushe Mh. Rais Samia Suluhu Hassan.
Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumanne, Mei 9, 2023) wakati akizungumza na viongozi wa serikali na chama, pamoja na watumishi wa wilaya ya Handeni waliohudhuria kikao cha siku Moja alichokiitisha wilayani Handeni akiwa na lengo la kujitambulisha kwao.
"Kwenye upendo kuna ustahimilivu na kusameheana, upendo washinda fitina, ubaya, ushirikina, na kila kitu kibaya. Mkiruhusu chuki, Halmashauri zenu hazitafanya kazi vizuri." amesema.
Kushoto, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Handeni Saitoti Zelothe Stephen na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Handeni Bi. Maryam Ahmad Ukwaju wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Tanga hayupo Pichani. Wengine, ni viongozi wa Halmashauri na Sekretarieti ya Mkoa wa Tanga.
Akiwa wilayani Handeni, Mh. Kindamba amempongeza Mkurugenzi wa Handeni Mji Bi.Maryam Ukwaju kwa kufanya vizuri kwenye ukusanyaji mapato, pamoja na kuwataka wakurugenzi wa Halmashauri zote mbili kujali stahiki mbalimbali za watumishi wao ili kuwaongezea ari ya ufanyaji kazi.
Akihitimisha ziara yake ya siku Moja wilayani Handeni, Mkuu wa Mkoa amewataka viongozi wote wa Halmashauri kuwekea mkazo ukusanyaji wa mapato, kero za wananchi zitatuliwe kwa wakati na kwenye ngazi husika kabla ya kupelekwa ngazi za juu, pamoja na kupambana na ubadhilifu wa kwenye fedha ya umma.
Mkuu wa wilaya ya Handeni Wakili Albert Msando akizungumza mbele ua Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mh. Waziri Kindamba kwenye ukumbi wa FDC, Handeni Mji.
Awali, akimkaribisha Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa wilaya ya Handeni Wakili Albert Msando alimueleza Mkuu wa Mkoa kuwa katika miradi ya ujenzi wa shule mpya na madarasa unaoendelea, TAKUKURU wilaya ya Handeni wameanza zoezi la kupitia hati shindani za manunuzi ili kuhakikisha bei za vifaa vya ujenzi vinanunuliwa bila udanganyifu wa kupandisha bei za vifaa hivyo, lengo likiwa ni kuzuia ubadhilifu kwenye fedha za umma unaoweza kujitokeza.
Barabara ya Korogwe - Handeni
Anuani ya Posta: S.L.P 51 HANDENI
Simu ya Mezani: 027-2641807
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: td@handenitc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.