Mkuu wa Mkoa wa Tanga , Mhe Martine Shigela ameipongeza Wilaya ya Handeni kuwa ya Kwanza kutekeleza agizo lake la kutenga muda maalum wa kusikiliza na kutatua kero mbali mbali za Wananchi.
Shigela ametoa kauli hiyo leo Desemba 13, 2019 wakati akiwahutubia wakazi wa Handeni waliojitokeza kwa wingi kwenye viwanja vya Handeni Square kupata huduma mbalimbali za kijamii pamoja na kupatiwa ufumbuzi wa kero mbali mbali kwenye tukio la "Handeni One Stop Jawabu" iliyoanza toka tarehe 09 - 13 Desemba, 2019.
Katika tukio hilo Taasisi za Umma pamoja na binafsi zimejitokeza kwa wingi, taasisi za Umma zilizojitokeza kuhudumia Wananchi ni NIDA, RITA, TANESCO, TCRA, NHIF, MADINI, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Uhamiaji, TARURA, RUWASA, TTCL, pamoja na Idara za Halmashauri zote mbili yaani Halmashauri ya Mji na Wilaya Handeni.Taasisi binafsi zilizojitokeza ni NMB, CRDB, VODACOM, TIGO,
Vile vile Mkuu wa Mkoa ameagiza utaratibu wa kusikiliza kero za Wananchi ushuke mpaka ngazi za chini kuanzia Tarafa, Kata, Mtaa pamoja na vitongoji huku akisisitiza Watumishi wa Umma kuwajali wananchi kwa kuwasikiliza kero na kutotoa kauli zenye kuudhi pindi wanapotoa huduma.
Akitoa taarifa ya tathimini ya zoezi hilo Mkuu wa Wilaya ya handeni mhe.Godwin Gondwe kwanza amewapongeza watumishi wote waliofanikisha zoezi hilo bila kusahau wafanyabiashara ,amesema jumla ya takribani watu 35,000 wamepatiwa huduma katika eneo hilo kuanzia tarehe 9-12 Desemba, 2019.
Mwenyeji wa Shughulia hii ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Handeni bw.Kenneth Haule amewashukuru sana Wananchi wa Handeni kwa kutoa ushirikiano wa kutosha toka zoezi hilo lilipoanza tarehe 9/12 mpaka leo tarehe 13/12/2019 "Mwanzo tulidhani tukio hili lingekuwa dogo lakini mpaka sasa tumegundua tukio hili ni kubwa sana takribani zaidi ya watu 34,000 wamehudumiwa" amesema Haule.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga mhe.Martine Shigela akipima uzito na Urefu wake kwenye tukio "Handeni One Stop Jawabu"
Mkuu wa Mkoa akisikiliza baadhi ya kero kutoka kwa baadhi ya Wananchi kwenye tukio la "Handeni One Stop Jawabu"
Baadhi ya picha za matukio mbali mbali kwenye kilele cha "Handeni One Stop Jawabu" kwenye viwanja vya Handeni Square.
Barabara ya Korogwe - Handeni
Anuani ya Posta: S.L.P 51 HANDENI
Simu ya Mezani: 027-2641807
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: td@handenitc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.