Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe.Martine Shigela ameipongeza Halmashauri ya Mji Handeni kwa kuendelea kupata hati safi. Ameyasema hayo kwenye Baraza maalum la Madiwani la kujadili na kupitia hoja za Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG).
"Mwaka huu kama Mkoa hatuji tu kwa maana kwenye Ukaguzi. Baada ya taarifa ya Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) kutolewa tuliitisha kikao cha Wakurugenzi,Weka hazina pamoja na Wakaguzi wa ndani ili kila Halmashauri kupata picha ya taarifa yao waliyoipata katika ripoti ya Mwaka huu," amesema Shigela.
Amesema Ofisi ya Mkuu wa Mkoa itaendelea kushirikiana kwa karibu na Halmashauri ili kuhakikisha hoja nyingi zinazoibuliwa na CAG zinapatiwa majibu kwa wakati ili zisijirudie kwa wakati mwingine maana imeonekana hoja nyingi zinajirudia kila mwaka.
Mbali na hilo,amepongeza jitihada zinazofanywa uongozi wa Halmashauri kwa kuendelea kusimamia vyema matumizi fedha za Serikali hasa zinazoguza maslahi wa Wananchi moja kwa moja mfano miradi ya maendeleao inayotekelezwa kwenye maeneo mbalimbali.
Vile vile ameigiza Halmashauri kuendelea kusimamia kwa makini kwenye suala la ukusanyaji wa mapato kwa kuhakikisha inadhibiti mianya yote ya ukwepaji kodi ikiwemo kuongeza mashine za kukusanyia ushuru kwa njia ya kielektroniki (POS) kutoka kumi na nne (14) za sasa mpaka thelathini (30).
Kuhusu Maji amesema anaipongeza Halmashauri kwa kuendelea kufanya ukarabati wa vituo vya kuchotea Maji kwa kuwawezesha Wananchi kupata huduma hiyo kwa urahisi,kwa kuliona hilo Serikali mwaka huu wa fedha imetenga zaidi ya bilioni 200 kwenye mradi HTM ambapo tayari tenda imetangazwa muda wowote kuanzia sasa ukarabati wa miundombinu ya Maji mjini Handeni utaanza.
Kuhusu Elimu amesema baada ya Serikali kundelea kutoa Elimu bila malipo wazazi wamekuwa na muitikio mkubwa wa kupeleka watoto Shule matokeo yake kumeibuka changamoto ya upungufu wa miundombinu ya Madarasa,Ofisi, Maabara pamoja na matundu ya vyoo.amewaomba wahe.Madiwani kuweka utaratibu wa kushirikisha jamii kwenye utatuzi wa changamoto hizo ikiwemo kuanzisha hata utaratibu wa michango.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halamshauri mhe.Twaha aliwapongeza wahe.Madiwani,wakuu wa Idara na Vitengo kwa kuiwezesha Halmashauri kuendelea kupata hati .
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigela akizungumza kwenye Baraza maalum la kujadili hoja za CAG
Mkurugenzi wa Halmashauri Bw.Kenneth Haule akitoa maelezo kwenye baraza la maalum la kujadili hoja za CAG
Mwenyeki wa Halmashauri Mhe.Twaha Mgaya akizungumza jambo kwenye Baraza hilo
Barabara ya Korogwe - Handeni
Anuani ya Posta: S.L.P 51 HANDENI
Simu ya Mezani: 027-2641807
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: td@handenitc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.