Ofisi ya Kamanda wa TAKUKURU wilaya ya Handeni, imefanya kikao na wasimamizi wa miradi ya ujenzi ya miundombinu ya shule inayo gharamiwa na serikali kupitia mradi wa BOOST.
Lengo la kikao hicho ni kuwaelekeza wasimamizi wa miradi hiyo taratibu mbalimbali zinazopaswa kufuatwa kuanzia hatua za awali za ujenzi mpaka mradi utakapokamilika.
Akizungumza wakati wa kikao hicho, Kamanda wa TAKUKURU Wilaya ya Handeni Richard Kapungu, alisema "Leo tunaelekezana katika hali ya kirafiki, uelewe majukumu yako, umeletewa fedha za serikali, zisimamie, kamati zisiingiliane, ukishindwa kutimiza majukumu yako, tutarudi kwako kwa sura nyingine".
Nae Afisa kutoka TAKUKURU, Mhandisi Patrick Katemba aliwasisitizia wasimamizi hao kuhakikisha kasi ya ukamilishaji miradi hiyo, iendane na ubora, na hivyo kamati zilizoundwa katika kila mradi zitambue kuwa zinategemeana, kulegalega kwa kamati moja ni kulegalega kwa mradi mzima.
Halmshauri ya mji Handeni imepatiwa kiasi cha shilingi bilioni 1.4 na serikali kuu kupitia mradi wa BOOST kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya shule za msingi na awali. Na ujenzi wa miundombinu hiyo kwenye maeneo mbalimbali umeshaanza na unaendelea kwa kasi.
Barabara ya Korogwe - Handeni
Anuani ya Posta: S.L.P 51 HANDENI
Simu ya Mezani: 027-2641807
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: td@handenitc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.