Wajumbe wa timu ya Uongozi wa Halmashauri (CMT) wakiongozwa na Mkuu wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu,Bi.Monica Andrew kwa niaba ya Mkurugenzi wametembelea eneo la Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Halmashauri katika eneo la Kata ya Kwenjugo.
Mara baada ya kuwasili katika eneo la Mradi na kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo wajumbe wameonyesha kuridhishwa na kasi ya ujenzi ya Wakala wa Majengo nchini Tanzania (TBA) wanaojenga jengo hilo na kuwataka waukamilishe Mradi huo kwa wakati kama ilivyopangwa.
Akitoa ufafanuzi wakati za ziara hiyo mhandisi wa Mradi huo amesema wamekuwa wanajitahidi kuhakikisha mradi unaenda kwa kasi inayokusudiwa ili waweze kukabidhi kwa wakati,mpaka sasa kazi ambazo zimeishafanyika toka wakabidhiwe eneo la mradi mnamo tarehe 10 Oktoba,2017 ni kama zifuatazo;-
i)Uchimbaji wa msingi wa ghorofa-hii imehusisha uondoaji wa sehemu ya Ardhi ilikupisha ujenzi wa msingi wa jengo.
ii)Bliding sehemu za column base na strips
iii)Umwagaji wa zege la kwenye vitako vya nguzo za wima
iv)Umwagaji zege la ground beams
v)Kuseti mitambo ya ukataji na ukunjaji chuma
vi)Umwagaji wa zege la kwenye strips
vii)Kurudisha udongo sehemu ya msingi wa jengo
viii)Mkanda wa kuunganisha nguzo
picha hapo juu zikionyesha hatua za mradi ulipofikia
Barabara ya Korogwe - Handeni
Anuani ya Posta: S.L.P 51 HANDENI
Simu ya Mezani: 027-2641807
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: td@handenitc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.