Leo Alhamisi ya tarehe 06 Julai 2023, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Handeni Bi.Maryam Ukwaju amepokea gari moja lenye namba ya usajili STM 6066, kupitia mradi wa EP4R kwa ajili ya Idara ya Elimu Sekondari, ikiwa ni awamu ya nne ya ugawaji wa magari kwenye Halmashauri zote nchini.
Akizungumza baada ya kuwasili kwa gari hilo Afisa Elimu Sekondari Mwl.Mtendeje Kingimali, ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa namna ambavyo inatoa fedha mbalimbali za miradi ya maendeleo kwenye sekta ya Elimu, kwa kuipatia Halmashauri ya Mji Handeni gari itakayorahisisha na kuongeza ufuatiliaji wa masomo, ufundishaji, ujenzi na usimamizi wa miundombinu kwenye shule.
Mwl. Mtendeje Kingimali alihitimisha kwa kuahidi wazazi, walezi na wananchi wa Halmashauri ya Mji Handeni, kutarajia kazi kubwa yenye ufanisi itakayokwenda kufanyika kutokana na kuwepo wa gari hilo litakaloongeza nguvu ya ufuatiliaji wa shughuli katika shule za sekondari.
Barabara ya Korogwe - Handeni
Anuani ya Posta: S.L.P 51 HANDENI
Simu ya Mezani: 027-2641807
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: td@handenitc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.