Wakuu wa Shule za msingi na Sekondari pamoja na waratibu Elimu Kata katika Halmashauri ya Mji Handeni wameshiriki mafunzo ya mfumo wa malipo na kutoa taarifa za Fedha za vituo vya kutoa huduma (FFARS-Facility Financial Accounting Reporting System) kwa muda wa siku tatu yaani tarehe 12,13 na 17 mwezi wa kumi (10) mwaka 2017.
Mfumo huu utasaidia kuongeza uwazi na uwajibikaji kwa watumishi hasa eneo la mapokezi na matumizi ya Fedha za Umma.Hii ni kuanzia katika vituo vya kutolea huduma za Elimu na Afya mpaka katika ngazi ya Halmashauri.
Aidha,kwa kuzingatia Sera ya Ugatuaji wa Madaraka kwa wananchi ( D by D ) na kupitia utaratibu wa Serikali Kuu kupeleka Fedha za matumizi ya kawaida na shughuli za maendeleo moja kwa moja katika vituo vya kutolea huduma za Elimu na Afya,mfumo huu utasaidia kusimamia mapato na matumizi sahihi ya Fedha za Serikali na kuleta maendeleo ya haraka kwa wananchi.
Barabara ya Korogwe - Handeni
Anuani ya Posta: S.L.P 51 HANDENI
Simu ya Mezani: 027-2641807
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: td@handenitc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.