• Wasiliana na sisi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Handeni Town Council
Handeni Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Handeni

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Fedha na Biashara
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Elimu Msingi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Maji
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Ardhi na Maliasili
      • Elimu Sekondari
      • Usafi na Mazingira
    • Vitengo
      • Teknolojia,Habari na Mawasiliano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Ugavi
      • Nyuki
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya kitalii
    • kilimo
    • ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za Kudumu za Halmashauri
      • fedha na uongozi
      • mipango miji na mazingira
      • uchumi afya na elimu
      • ukimwi
      • maadili
    • Ratiba
      • vikao vya waheshimiwa madiwani
      • kuonana na mwenyekiti
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Miongozo Mbalimbali
    • fomu mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za Shughuli za Ofisi au Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha
    • Matukio

Walimu Halmashauri ya Mji Handeni, wapata mafunzo ya mfumo wa PReM

Posted on: April 14th, 2023

Leo Ijumaa Tarehe 14/04/2023 Baraza la mitihani Tanzania(NECTA) limehitimisha mafunzo ya siku mbili kuhusu mfumo wa kielektroniki wa utunzaji wa taarifa za wanafunzi(PReM), kwa walimu wa shule za msingi Halmashauri ya Mji Handeni. Katika mafunzo hayo mada mbalimbali zilifundishwa ikiwemo namna ya kujaza taarifa za wanafunzi, namna ya kufanya uhamisho wa wanafunzi kutoka shule moja Kwenda nyingine pamoja na namna ya kutumia mfumo huo kwa kufuata taratibu zote za kiusalama wa taarifa hizo. Mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbiwa chuo cha maendeleo ya wananchi FDC yamehudhuriwa na wataalamu mbalimbali kutoka Baraza la mitihani Tanzania(NECTA), Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Handeni, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Handeni, Maafisa Elimu msingi, Maafisa Tehama wa Halmashauri ya Mji Handeni, wakuu wa shule na watakwimu wa shule zote za msingi za Halmashauri ya Mji Handeni

Katika mafunzo hayo ndugu Sadick Manjoti mtaalam wa Tehama kutoka Baraza la mitihani Tanzania(NECTA), amewataka walimu kuchukua tahadharij juu ya usalama wa taarifa za wanafunzi wanazoziweka katika akaunti zao, dhidi ya wadukuzi wa aina tofauti ambao wanaweza kupelekea upotevu na uharibifu wa taarifa au upatikanaji wa taarifa kwa wasiohusika.

Walimu wakuu na watakwimu wa shule za msingi Halmashauri ya Mji Handeni, wakifuatilia kwa makini mafunzo ya  mfumo wa utunzaji wa taarifa za wanafunzi(PReM)

Kwa upande wake Bi.Asha Hemedi, Afisa usajili kutoka Baraza la mitihani Tanzania(NECTA), amewataka walimu hao kuhakikisha wanajaza taarifa za wanafunzi mapema ili kuweza kupata muda wakutosha, kupitia upya na kuhakiki taarifa hizo ili kuepusha taarifa zisizosahihi, ambazo huathiri bajeti ya shughuli za uendeshaji wa  zoezi la mitihani kwa shule husika.

Mtakwimu wa shule ya msingi Mpakani Mwalimu. Saumu Magongo, akiuliza swali katika mafunzo ya mfumo wa utunzaji wa taarifa za wanafunzi(PReM)

Nae Afisa Elimu msingi wa Halmashauri ya Mji Handeni ndugu Shomari Bane, amewataka walimu kuzingatia muda wa kujaza taarifa za wanafunzi ili kuepusha ucheleweshaji wa taarifa, pamoja na hivyo ndugu Shomari Bane amemshukuru Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dokta. Samia Suluhu Hassan, kuwawezesha walimu kwa kuwapatia vishikwambi, ambavyo vimekuja kutatua changamoto ya uhaba wa vifaa vya Tehama, hivyo wanaweza kutumia mifumo mbalimbali kwa urahisi na kwa wakati husika kutokana na vishikwambi hivyo.

Mheshimiwa.Mussa Mkombati akizungumza na walimu wa shule za msingi Halmashauri ya Mji Handeni, katika mafunzo ya mfumo wa utunzaji wa taarifa za wanafunzi(PReM) yaliyofanyika katika ukumbi wa chuo cha maendeleo ya wananchi (FDC)

Akizungumza na walimu waliohudhuria katika mafunzo hayo Mwnyekiti wa Halmashauri ya Mji Handeni Mheshimiwa.Mussa Mkombati, amewasihi walimu kujiepusha na suala la udanganyifu wa mitihani, kwani serikali ipo makini na haitafumbia macho suala hilo, pia amewataka  walimu wajiepushe na udanganyifu katika takwimu za wanafunzi,  kuzihakiki upya na kurekebisha pale ambapo zina makosa. Mheshimiwa.Mussa Mkombati amewataka walimu na watendaji wote wa shule kupambana katika kuwezesha wanafunzi kuwa na uwezo wa kujua kusoma, kuandika na kuhesabu, kufuta utoro na kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula wakiwa shuleni  pia amewasisitiza walimu kushirikiana na viongozi wa serikali za mitaa na kata husika wakati wanapofanya mikutano yao, ambao viongozi hao ndio wasimamizi wakuu wa maadhimio ya mikutano hiyo.

 Nae Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Handeni Bi. Maryam Ukwaju, amewasisitiza walimu juu ya kufuata taratibu sahihi za matumizi ya mfumo wa FFARS, ambao ndio mfumo pekee wa ufanyaji malipo ili kuepusha hoja katika kipindi cha ukaguzi, pia amewataka kuzingatia taratibu zote za kuomba fedha za uhamisho kwani ni haki ya kila mtumishi pale anapohamia makazi mapya katika utumishi wake na kujiepusha na tabia za kughushi barua za uhamisho, akihitimisha Bi.Maryam Ukwaju amewataka walimu kusaidiana na wazazi  kuwalea watoto katika maadili mazuri ili kudhibiti tatizo la mmomonyoko wa maadili katika Jamii.


Abdulkadir Kassim

Handeni Mji

Matangazo

  • KUITWA KWENYE USAILI 2 October 03, 2024
  • KUITWA KWENYE USAILI 1 September 27, 2024
  • TANGAZO LA MAJINA NA MIPAKA YA MITAA September 16, 2024
  • Angalia zaidi

Habari Mpya

  • HOSPITALI YA HALMASHAURI YA MJI HANDENI IMETOA ELIMU YA KUJINGA KWA MAGONJWA YA KUAMBUKIZA KWA WAFANYAKAZI WA BOMBA LA MAFUTA WILAYA YA HANDENI EACOP

    March 21, 2025
  • BARAZA MAALUMU LA MADIWANI LAPENDEKEZA KUONGEZEWA MAENEO YA UTAWALA

    March 14, 2025
  • MKUTANO MKUU WA 39 WA JUMUIYA YA TAWALA ZA MITAA TANZANIA (ALAT)

    March 11, 2025
  • ZIARA YA MHE. RAIS DKT SAMIA SULUHU HASSAN

    February 25, 2025
  • Angalia zaidi

Video

Mbunge wa jimbo la Handeni Mjini Mh.Reuben Kwagilwa aliamsha Bungeni
More Videos

Viunganishi vya Haraka

  • Dira na Dhamira
  • Kupata leseni ya Biashara
  • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
  • Kumuona Mkurugenzi
  • Kupata kibali cha Matangazo
  • Muundo wa Tasisi
  • Kumuona Mwenyekiti wa Halmashauri

Viunganishi Linganifu

  • Sekretariti ya Ajira
  • Ofisi ya Rais - Ikulu
  • FFARS-LIVE
  • PLANREP- BAJETI 2020/21
  • TAMISEMI
  • Utumishi

Watembeleaji wa Dunia

world map hits counter

Idadi ya waliotembelea tovuti

free HitCounter

Ramani

Wasiliana na sisi

    Barabara ya Korogwe - Handeni

    Anuani ya Posta: S.L.P 51 HANDENI

    Simu ya Mezani: 027-2641807

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: td@handenitc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.