Wataalamu toka Ofisi ya Rais TAMISEMI wameendesha mafunzo ya mifumo ya TEHAMA Serikalini kwa watumishi wa kada tofauti ambao moja kwa moja wanahusika na mifumo hiyo.
Mafunzo hayo yamelenga mfumo wa kuandaa mpango na bajeti (PlanRep),mfumo wa usimamizi wa matumizi ya fedha za umma kwenye vituo vya kutolea huduma (FFARS),mfumo wa ukusanyaji mapato kwa njia ya kielektroniki (LGRCIS).Lengo la mafunzo haya ni kutatua changamoto zinazojitokeza wakati wa matumizi ya mifumo hii ili kuweza kuwarahisishia watumiaji kutimiza majukumu yao kwa ufanisi.
Mafunzo hayo yataendeshwa kwa muda wa siku mbili kuanzia tarehe 22/01/2018 mpaka tarehe 23/01/2018 ili kuwapa nafasi ya kutosha watumiaji wa mifumo hiyo kutoa changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo kwa wataalamu hao ili waweze kuzitatua kwa wakati na kuleta ufanisi kwenye utoaji huduma kwa Wananchi kama ilivyo sera ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Picha mbalimbali hapo juu zikionyesha washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia kwa makini.
Barabara ya Korogwe - Handeni
Anuani ya Posta: S.L.P 51 HANDENI
Simu ya Mezani: 027-2641807
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: td@handenitc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.