Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Elimu) Dkt. Charles Msonde amefanya ziara ya siku moja ya kikazi katika Halmashauri ya Mji HANDENI, kwenye miradi ya ujenzi wa shule na madarasa katika kata ya Kwamagome na Kwenjugo, ambapo alitembelea na kukagua jumla ya miradi minne ambayo miwili ni ya ujenzi wa shule mpya ya sekondari Togeza iliyopo katika kata ya Kwamagome na shule mpya ya sekondari ya Mapinduzi iliyopo katika kata ya Kwenjugo. Miradi mingine miwili ni ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na vyumba vya maabara katika shule ya sekondari Msaje na ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya sekondari Kwenjugo.
Aidha ameelekeza kuwa pesa za miradi ya ujenzi wa madarasa ya shule za sekondari ya Msaje na shule ya sekondari ya Kwenjugo ambazo tayari serikali imeshazituma zitumike kwa ajili ya kumalizia miradi ya majengo ya shule hizo kama ilivyokusudiwa, hata hivyo kwakuwa serikali inatambua juhudi za wananchi walizozifanya za kuanzisha miradi ya shule mbili mpya za sekondari, hivyo basi serikali iko tayari kuunga mkono juhudi hizo.
Wakati huohuo Mkuu wa wilaya ya Handeni Bi.Sirieli Mchembe akizungumza mbele ya wananchi, amemshukuru Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Elimu) Dkt. Charles Msonde kwa kuweza kutenga muda, kuja kutembelea na kujionea miradi ya maendeleo inayofanywa katika wilaya yake na kumuahidi kuwa maelekezo yake aliyoyatoa yamezingatiwa na yatafanyiwa kazi.
Abdulkadir Kassim
Handeni Mji
Barabara ya Korogwe - Handeni
Anuani ya Posta: S.L.P 51 HANDENI
Simu ya Mezani: 027-2641807
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: td@handenitc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.