Halmashauri ya Mji Handeni leo tarehe 21/10/2017 imeanza rasmi kugawa maeneo kwa ajili ya ujenzi wa vibanda vya biashara eneo la soko jipya Seuta.
Baadhi ya Wananchi waliotuma maombi yao kwa Mkurugenzi wa Mji wamejitokeza ili waweze kuonyeshwa maeneo ya ujenzi wa vibanda vya biashara.Kabla ya zoezi la ugawaji wa maeneo halijaanza mwanasheria wa Mji Bw.Richard Unambwe amesisitiza kuwa zoezi la ugawaji wa maeneo linawahusu tu wananchi waliotuma barua za maombi kwa Mkurugenzi wa Mji na si vinginevyo,vilevile amesisitiza kila mtu kuwa makini na eneo atakaloonyeshwa ili kuondoa uwezekano wa watu au mtu kuvamia eneo lisilo la kwake.
Zoezi la ugawaji wa maeneo ya ujenzi wa vibanda vya biashara kwenye eneo la soko jipya la Seuta ni endelevu mpaka hapo eneo lote litakapojaa,hivyo wananchi wote wenye nia ya ujenzi wa vibanda vya biashara wanasisitizwa kuendelea kutuma maombi yao kwa Mkurugenzi wa Mji.
Wataalam wa Halmashauri ya Mji Handeni wakipitia baadhi ya nyaraka kabla ya zoezi kuanza
Wananchi wakisubiri maelekezo kutoka kwa wataalam wa Halmashauri ya Mji Handeni
Bw.Richard Unambwe Mwanasheria wa Halmashauri akifafanua jambo
Wananchi wakisikiliza kwa makini maelekezo kabla ya zoezi kuanza
Barabara ya Korogwe - Handeni
Anuani ya Posta: S.L.P 51 HANDENI
Simu ya Mezani: 027-2641807
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: td@handenitc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.