Uongozi: Halmashauri imejipanga kutoa kiwango cha juu kabisa cha uongozi wa kiraia na utendaji bora kwa ajili ya kuboresha maisha ya jamii yetu
Ushirikishwaji wa Jamii: Halmashauri inahimiza ushiriki na ushirikiano wa jamii katika shughuli za Halmashauri na kuthamini mchango wa kila mtu katika masuala ya uongozi, utoaji wa huduma, uibuaji na utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Usawa na Uwazi: Uthabiti na uwazi ni msingi muhimu katika maamuzi na taratibu za Halmashauri ili kuhakikisha haki kwa sekta zote za jamii.
Ubora: Halmashauri inalenga kuboresha kwa kuendeleza tija, huduma, miundombinu na taratibu zake, na kujenga sifa ya umahiri ndani ya uwezo wake wa kifedha ili kuinua ubora wa maisha ya jamii kwa njia endelevu kiuchumi.
Uharaka wa Majibu: Halmashauri inalenga kujibu kwa haraka mahitaji na matarajio ya wananchi wake.
Maendeleo Endelevu: Halmashauri imejizatiti kusimamia ipasavyo mali na miundombinu yake ili kuwezesha maendeleo yanayozingatia uchumi, mazingira na ustawi wa kijamii kwa manufaa ya jamii.
Uwazi wa Masharti: Halmashauri itahakikisha kwamba, kadiri itakavyowezekana, Kanuni, Sheria ndogo na taratibu zake za utekelezaji ni rahisi, wazi na sahihi.
Uwajibikaji: Halmashauri itatekeleza na kuendesha shughuli zake za kila siku kwa mujibu wa Sheria kutegemeana na uwezo wa kifedha kwa wakati huo ili kuhakikisha maendeleo endelevu kwenye jamii husika.
Wajibu: Halmashauri itasimamia wadau wake wakiwemo Watumishi, Madiwani na wadau wengine wa maendeleo ili kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa ufanisi, bidii, nidhamu na uaminifu.
Migongano ya Maslahi: Madiwani na watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Handeni watatakiwa kujiepusha na migongano ya maslahi binafsi katika shughuli za Halmashauri, watatakiwa kujiongoza na kujituma na kutii sheria za nchi katika utekelezaji wa majukumu yao.
Barabara ya Korogwe - Handeni
Anuani ya Posta: S.L.P 51 HANDENI
Simu ya Mezani: 027-2641807
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: td@handenitc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.