Mkutano wa kwanza wa Baraza la pili la Madiwani umefanyika leo tarehe 29.01.2021.
Kabla ya kuanza kwa Mkutano huo kulitanguliwa na Baraza la kujadili maendeleo ya Kata ambapo kila Diwani aliwasilisha shughuli zilizotekelezwa kwa kipindi husika pamoja na malengo waliojiwekea kuhakikisha shughuli nyingi za maendeleo zinakweda kwa kasi.
Kamati mbalimbali zimewasilisha shughuli za utekelezaji wa miradi ya maendeleo, kamati hizo ni kamati ya fedha na Uongozi, Huduma za Jamii, Ukimwi pamoja na Mipango Miji.
Akizungumza kwenye mkutano huo Mwenyekiti wa Halmashauri mhe.Mussa Mkombati amewaomba wahe.Madiwani pamoja na Wataalam kutokaa Ofisini watumie muda wao mwingi kutembelea maeneo mbalimbali ili kusikiliza kero za Wananchi na kuweza kuzitatua kwa haraka.
kuhusu Elimu Baraza limejipanga kuhakikisha kila mtoto anayestahili kwenda Shule anakwenda, pia kuhakikisha mapambano ya mimba kwa wanafunzi zinadhibitiwa na ikabainika wale wote wanaohusika sheria ichukue mkondo wake.
Akizungumza kwenye baraza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Bw.Kenneth Haule amewaomba wahe.Madiwani kuwasimamia kwa karibu Watendaji wote wa Serikali waliyopo ngazi za Kata na Mitaa kuhakikisha wanawasilisha taarifa za utekelezaji wa shughuli mbali mbali kwenye maeneo yao ili kuweza kuondoa baadhi ya kero zilizopo ngazi ya Kata na Mitaa kuliko kusubiri vikao vikubwa vya maamuzi.
Barabara ya Korogwe - Handeni
Anuani ya Posta: S.L.P 51 HANDENI
Simu ya Mezani: 027-2641807
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: td@handenitc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.