Kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Toba Nguvila, Afisa Tarafa wa Chanika Bw.Lusonge amezindua mpango wa Uandikishaji na utoaji wa Vyeti vya Kuzaliwa bure kwa watoto chini ya miaka mitano, uzinduzi huo umefanyika leo tarehe 10.08.2020 katika viwanja vya Zahanati ya Chanika. Katika uzinduzi huo wazazi wenye watoto chini ya umri wa miaka mitano wamepatiwa vyeti vya kuzaliwa bure.
Katika hotuba yake Mkuu wa Wilaya iliyosomwa na Afisa Tarafa amesema "Kwanza nianze kusema ni haki ya Mtoto kutambuliwa lakini zaidi ya hapo akishatambuliwa lazima apate nyaraka ya uthibitisho ya kutambuliwa kwake ambayo ni Cheti cha Kuzaliwa. Kwa wasiojua Cheti cha Kuzaliwa ni nyaraka ambayo kisheria hutumika kuthibitisha taarifa muhimu sana kwa mmiliki wa cheti hicho na hutumika maeneo mbalimbali kupata huduma za kijamii. Cheti cha kuzaliwa kina matumizi mengi, hutumika katika kuandikisha watoto wanaoanza Elimu ya Msingi na wale wanaojiunga na Elimu ya Sekondari na sasa hivi huwezi kupata nafasi ya kujiunga Elimu ya juu pamoja na kupata mikopo kwa ajili ya masomo hayo. Vile vile Cheti cha Kuzaliwa ni kiambatanisho cha Msingi ili kupata nyaraka nyingine za utambulisho kama kadi ya Kupiga Kura, Kitambulisho cha Taifa, pasi ya kusafiria, leseni ya Udereva kote huku utataikiwa kuwa na Cheti cha Kuzaliwa ili kuthibitisha mahali na tarehe uliyozaliwa".
Wazazi/Walezi wa Watoto Chini ya Miaka wakiwa kwenye hafla ya Uzinduzi Viwanja vya Zahanati ya Chanika
Afisa tarafa ya Chanika kwa niaba ya Mkuu Wilaya akifanya uzinduzi
Mzazi akipokea cheti cha Kuzaliwa cha Mtoto wake Wakati wa Uzinduzi
Kikundi cha Ngoma za Asili kutoka magamba kikitoa burudani wakati wa hafla ya Uzinduzi
Bw.Gerad Kauki Afisa Maliasili akisoma hotuba ya uzinduzi kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Handeni Bw.Kenneth Haule.
Barabara ya Korogwe - Handeni
Anuani ya Posta: S.L.P 51 HANDENI
Simu ya Mezani: 027-2641807
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: td@handenitc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.