Baraza la Madiwani Halmashauri ya Mji Handeni kwa pamoja limeridhia wahe.Madiwani wote kukatwa posho yao ya Mwezi ili kuchangia miradi mbalimbali ya Maendeleo.
Akizungumza kwenye kikao cha Baraza la madiwani cha tarehe 27/11/2018 kujadili taarifa za kamati za kudumu Robo ya kwanza 2018/2019 Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe.Twaha Mgaya ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kwenjugo amependekeza kwa Baraza hilo kuona jinsi ya kuungana na Wananchi pamoja na Serikali kwenye utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Maendeleo.
Ambapo amependekeza kila mhe.Diwani akubali kukatwa posho yake ya Mwezi mmoja ili kuchangia kwenye utekelezaji wa miradi ya maendeleo hasa kwenye sekta za Afya na Elimu, mara baada ya kutoa pendekezo hilo aliwahoji wahe.Madiwani kama wameafiki ambapo kwa pamoja wote wamekubali kukatwa posho zao.Aidha Mwenyekiti amesisitiza kuwa posho hiyo siyo lazima ikatwe kwa pamoja mara moja Diwani anaweza kuamua kuwa anachangia kidogo kidogo mpaka afike kile kiasi cha posho anachokipata kwa mwezi, lakini ahakikishe anakamilisha mchango wake kabla ya Uchaguzi wa mwaka 2020.
Baadhi ya Waheshimiwa Madiwani wakipitia taarifa mbalimbali wakati wa Baraza la Robo ya kwanza 2018/2019 likiendelea tarehe 27/11/2018
Akizungumza wakati wa hoja hiyo Mhe.Ulenge Diwani wa Kata ya Mdoe amesema wao Madiwani wamekuwa wakichangia shughuli nyingi za maendeleo katika maeneo yao hivyo haoni haja ya kwa nini wasikatwe posho zao ili kuendelea kuwatia moyo Wananchi wanaojitoa kwa hali na mali kuhakikisha maendeleo yanapatikana kwenye maeneo yao.
Wakati huo huo Baraza limeridhia na kuwadhibitisha Wakuu wa Idara na Vitengo nane (08), ambao ni :-
1)Bw.Thomas Mzinga - Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii
2)Bw.Omari Mashaka - Mkuu wa Idara ya Elimu Msingi
3)Bi.Mtendeje Kingimali - Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari
4)Bw.Fabian Massawe - Mkuu wa Idara ya Fedha na Biashara
5)Bw.Richard Unambwe - Mkuu wa Kitengo cha Sheria.
6)Dkt.Feisal Said - Mkuu wa Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
7)Bw.Wilbard Sakaya - Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi
8)Bw.Oscar Myovela - Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
Barabara ya Korogwe - Handeni
Anuani ya Posta: S.L.P 51 HANDENI
Simu ya Mezani: 027-2641807
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: td@handenitc.go.tz
Copyright ©2022 GWF . All rights reserved.